Na Saulo Stephen - Singida.
Kuimarisha lishe bora, hususan katika shule za msingi na sekondari, kumetajwa kuwa miongoni mwa hatua muhimu za kupunguza hali ya lishe duni na kuhakikisha wananchi, hususan watoto, wanakuwa na afya njema.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, wakati wa kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe kwa robo ya nne kuanzia Aprili hadi Juni 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Manispaa ya Singida.

Gondwe amesema juhudi za utekelezaji wa afua za lishe zinapaswa kuendelezwa kwa kuzingatia ushirikiano wa wadau mbalimbali, ili kuhakikisha watoto na wananchi kwa ujumla wanapata lishe bora na yenye afya.
Kikao hicho kiliwakutanisha wajumbe mbalimbali, wakiwemo Watendaji wa Kata, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Waratibu wa Maendeleo ya Afya ya Mama na Mtoto, waratibu wa lishe, afya ya uzazi, mama na mtoto, pamoja na wawakilishi kutoka Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Bi. Ester Chaula, amewasihi wajumbe wote kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuongeza juhudi katika maeneo ya kazi ili kuhakikisha hali ya lishe katika halmashauri inaendelea kuimarika.
Discussion
Reader comments
0 contributions