Skip to main content

UHALIFU: WATUHUMIWA 95 WAKAMATWA SINGIDA

Jumla ya watuhumiwa 95 wamekamatwa katika operesheni mbalimbali za kupambana na uhalifu zilizofanyika mkoani Singida mwezi Septemba 2026.

UHALIFU: WATUHUMIWA 95 WAKAMATWA SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

UHALIFU: WATUHUMIWA 95 WAKAMATWA SINGIDA

0:00 --:--

Jumla ya watuhumiwa 95 wamekamatwa katika operesheni mbalimbali za kupambana na uhalifu zilizofanyika mkoani Singida mwezi Septemba 2026.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amon Kakwale, amesema watuhumiwa hao wanahusishwa na makosa mbalimbali ya jinai, yakiwemo mauaji, wizi, dawa za binadamu na wizi wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu pamoja na mali nyingine zinazodaiwa kupatikana kwa njia ya wizi.

Aidha, operesheni hizo zimehusisha watuhumiwa wa unyang’anyi wa kutumia silaha, kuvunja nyumba na wizi wa vifaa vya kielektroniki, huku wengine wakikamatwa kwa makosa mengine ya jinai.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limesema litaendelea na operesheni hizo kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao, huku likiwataka wananchi kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini na kukamata wahalifu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.