Skip to main content

UHALIFU: SITA WAHUKUMIWA KUNYONGWA KWA HATIA YA MAUAJI TABORA

Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu 18 kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo mauaji, biashara ya dawa za kulevya pamoja na kumiliki silaha kinyume cha Sheria kufuatia msako na doria zilizofanywa kati ya Juni na Julai 2026.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP. Twaha Lulengelule amesema miongoni mwa waliokamatwa, Watu sita wamepatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia na wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Waliohukumiwa ni pamoja na Majuti Lutema (32), Soda Mayeka (47), Kulwa Masunga Senga (44), Iddy Ramadhani (35), Chandika Fideli (36) na Mussa Marko (28).

Watuhumiwa wanne walikamatwa wakimiliki silaha aina ya Rifle Model 70-458 isiyo na namba za usajili pamoja na risasi tatu bila kibali maalum, huku wengine tisa wakikamatwa na bangi kilo 117.2062.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.