Na Pascal Tuliano - Tabora.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao, amesema uchunguzi juu ya tukio la Moto katika Shule ya Sekondari ya Kaliua unaendelea, ili kubaini chanzo na tathmini ya hasara iliyopatikana.
SACP Abwao ameyasema hayo mara baada ya kufika katika Shule hiyo ya Sekondari Kaliua iliyopo wilayani Kaliua, kujionea uharibufu kufuatia tukio la moto lililozuka ndani ya bweni la Wasichana.

Tukio hilo limetokea Machi 23, 2026 na kuleta taharuki kwa Wanafunzi na uongozi wa shule hiyo, ambapo kwa mujibu wa taarifa za awali, moto huo haukuleta madhara yoyote kwa Wanafunzi na Walimu.
Hata hivyo, inqqrifiwa kuwa uharibifu wa mali ni mkubwa, ambapo miundombinu ya bweni pamoja na mali binafsi za wanafunzi ziliteketea, huku SACP Abwao akitoa pole kwa uongozi wa shule, wanafunzi na wazazi kwa tukio hilo.

Miongoni mwa vitu vilivyoathirika ni pamoja na magodoro, nguo, vitabu na madaftari ya wanafunzi, hali iliyowaacha wengi wao katika wakati mgumu wa kuendelea na masomo yao. Uongozi wa shule unaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wanafunzi wanaathirika wanapata msaada unaohitajika.



Discussion
Reader comments
0 contributions