Skip to main content

UBUNIFU MAONESHO YA NANENANE TABORA WAMPA TABASAMU DC MONGELLA

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Gerald Mongella, amepongeza ubunifu na matumizi ya teknolojia mbalimbali yanayooneshwa katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Magharibi yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Fatma Mwasa, Ipuli, Manispaa ya Tabora.

UBUNIFU MAONESHO YA NANENANE TABORA WAMPA TABASAMU DC MONGELLA

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Gerald Mongella, amepongeza ubunifu na matumizi ya teknolojia mbalimbali yanayooneshwa katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Magharibi yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Fatma Mwasa, Ipuli, Manispaa ya Tabora.

Dkt. Mongella ametoa pongezi hizo alipofanya ziara ya kutembelea mabanda ya washiriki wa maonesho hayo akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Anthony Mwakisu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, IGP Mstaafu, Balozi Simon Sirro.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mongella amevutiwa na bidhaa mbalimbali zilizokuwa zinazooneshwa, hususan samani za ofisini na majumbani zinazozalishwa na Jeshi la Magereza. Alisifu ubora wa samani hizo pamoja na ufundi stadi uliotumika katika utengenezaji wake, akieleza kuwa zina uwezo mkubwa wa kushindana katika soko.

Aidha, amewahimiza Jeshi la Magereza kuongeza uzalishaji wa samani hizo ili kukidhi mahitaji ya soko linalozidi kukua na kuchangia zaidi katika maendeleo ya sekta ya viwanda nchini.

Sambamba na hilo, Dkt. Mongella amewakaribisha kuwekeza katika Wilaya ya Kaliua kwa kutumia fursa ya upatikanaji wa malighafi za mbao, akibainisha kuwa wilaya hiyo ina rasilimali za kutosha zinazoweza kusaidia kukuza uzalishaji wa samani na shughuli nyingine za viwanda vinavyotegemea mazao ya misitu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.