Skip to main content

UBORA WA BIDHAA NI NGUZO MUHIMU YA USHINDANI WA SOKO LA NDANI, KIMATAIFA - TBS

Na Gideon Gregory - Dodoma.

UBORA WA BIDHAA NI NGUZO MUHIMU YA USHINDANI WA SOKO LA NDANI, KIMATAIFA - TBS

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema ubora wa bidhaa ni nguzo muhimu ya kuwafanya wafanyabiashara wa Tanzania kushindana katika soko la ndani na kimataifa, huku likisisitiza kuwa bidhaa zisizokidhi viwango haziwezi kudumu sokoni.

Akizungumza Agosti 5, 2026 katika Maonesho ya 33 ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma, Meneja wa TBS Kanda ya Kati Mwl. Hamis Mwanasala, amesema taasisi hiyo inaunga mkono kaulimbiu ya Nanenane ya mwaka huu "Tambua soko, ongeza tija kutekeleza dira 2050" kwa kuhakikisha wazalishaji wanazingatia viwango vya ubora ili kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania.

Meneja wa TBS Kanda ya Kati Mwl. Hamis Mwanasala.

"TBS inaendelea kutoa huduma za usajili wa bidhaa, uthibitishaji wa ubora pamoja na elimu kwa wazalishaji na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango vinavyotakiwa kabla ya bidhaa kufikishwa sokoni,"amesema.

Mwl. Mwanasala amesema ubora wa bidhaa huongeza imani ya walaji huimarisha biashara na kuongeza mapato kwa wazalishaji jambo linalochangia ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi kupitia ajira, elimu, afya na huduma nyingine za kijamii.

"TBS imeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kujenga maabara na kuimarisha mifumo ya upimaji katika maeneo mbalimbali nchini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za uthibitishaji wa ubora,"amesema.

Kuhusu bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi, amesema TBS hutumia mfumo maalum ambao huhakikisha bidhaa zinakaguliwa na kuthibitishwa zinakidhi viwango kabla ya kuingia katika soko la Tanzania.

Ameongeza kuwa pamoja na ukaguzi unaofanyika mipakani, TBS inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara sokoni ili kubaini na kuondoa bidhaa hafifu au bandia, huku akiwahimiza wananchi kutoa taarifa wanapobaini bidhaa zinazotiliwa shaka.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.