Na Daniel Gahu - Katavi.
Mahakama ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi imemuhukumu Jumanne Lukas (20) Mkazi wa Ilunde Wilaya ya Mlele kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili.
Hukumu hiyo imetolewa Machi 25, 2026 mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Andrea Njau, ambapo alieleza kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 08, 2025 huko katika kijiji cha Ilunde saa tisa alasiri, ambapo alimlubuni mwanafunzi huyo kwa kumpeleka kwenye nyumba ya kulala wageni (Guest) kwa lengo la kujistarehesha.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 01, 2025 akikabiliwa na kosa la kubaka.
Njau aliendelea kueleza mshtakiwa huyo ametenda kosa hilo chini ya kifungu namba 130 sura ya 16 cha sheria ya kanuni ya adhabu kilichofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Aidha ameeleza kuwa mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri pasipo shaka uliotosha kumtia hatiani, mtuhumiwa.
Discussion
Reader comments
0 contributions