Skip to main content

TUTAENDELEA KUIMARISHA UPATIKANAJI HAKI KWA WENYE KIPATO CHA CHINI - DC GOWELE

Na Adam Msafiri - Mara.

TUTAENDELEA KUIMARISHA UPATIKANAJI HAKI KWA WENYE KIPATO CHA CHINI - DC GOWELE

Na Adam Msafiri - Mara.

Serikali imesema inaendelea kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wenye kipato cha chini kupitia huduma za msaada wa kisheria, sambamba na kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuripoti kwa usahihi masuala ya haki za binadamu na ukatili wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wanahabari wa Wilaya ya Tarime. Mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa na uwezo wa wanahabari katika kuripoti kwa weledi masuala ya upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meja Gowele amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kuhusu haki zao za msingi na huduma mbalimbali za kisheria zinazotolewa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Athuman Msosole, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanahabari kuripoti kwa usahihi matukio ya ukatili wa kijinsia, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na masuala mengine ya kijamii yanayohitaji uelewa wa kisheria.

Ameeleza kuwa wanahabari wenye uelewa wa masuala ya sheria wana nafasi kubwa ya kusaidia jamii kupata taarifa sahihi na kuongeza uelewa kuhusu namna ya kutafuta haki kupitia mifumo iliyowekwa na serikali.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Habari Wilaya ya Tarime, Jacob Karoli, ameziomba serikali na taasisi mbalimbali kuendelea kushirikiana na wanahabari katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya habari nchini.

Karoli amesema ushirikiano huo utasaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa wanahabari na kuongeza ufanisi katika utoaji wa taarifa zinazochochea maendeleo ya jamii.

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi pamoja na kuhakikisha taarifa zinazohusu haki za binadamu na msaada wa kisheria zinawafikia wananchi kwa usahihi kupitia vyombo vya habari.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.