Skip to main content

TUNATAMBUA MCHANGO WA RAIS SAMIA KATIKA KULETA MAENDELEO - CCM KIBAHA

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, kimesema kinaendelea kutambua mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo yanayoonekana kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

TUNATAMBUA MCHANGO WA RAIS SAMIA KATIKA KULETA MAENDELEO - CCM KIBAHA

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, kimesema kinaendelea kutambua mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo yanayoonekana kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 2, 2026 na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Pwani, David Mramba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho.

Amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, Mkoa wa Pwani ulitengewa Sh bilioni 47.3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, huku mwaka wa fedha 2026/2027 kiwango hicho kikiongezwa hadi Sh bilioni 497.1.

“Ongezeko hili linaonyesha wazi kuwa Mkoa wa Pwani upo moyoni mwa Rais Samia, na dhamira yake ni kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo,” amesema Mramba.

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Pwani, David Mramba.

Kwa upande wa sekta ya maji, amesema kuwa changamoto iliyokuwepo kwa muda mrefu imeanza kupungua kutokana na uwekezaji wa miradi mikubwa ya maji safi na salama, hali iliyosaidia kupunguza adha kwa wanawake na watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.

Ameeleza kuwa katika sekta ya elimu, Serikali imejenga madarasa mapya, maabara na kuboresha miundombinu ya vyoo, hatua iliyochangia wanafunzi kusoma katika mazingira bora zaidi.

Mramba amesema pia sekta ya afya imeimarika kupitia ujenzi wa zahanati na vituo vya afya pamoja na kuboreshwa kwa huduma za mama na mtoto, hali inayowawezesha wananchi kupata huduma karibu na makazi yao.

Akizungumzia miundombinu, amesema ujenzi na uboreshaji wa barabara umefungua fursa za kiuchumi kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao na kuongeza shughuli za biashara.

Amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya uongozi wa Rais Samia na jitihada za Serikali katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wa maeneo mbalimbali nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.