Skip to main content

TUMIENI UJIO WA MWENGE KAHAMA KUKUZA UCHUMI - KIGAILE

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

TUMIENI UJIO WA MWENGE KAHAMA KUKUZA UCHUMI - KIGAILE
Studio Narration JAMBO FM

TUMIENI UJIO WA MWENGE KAHAMA KUKUZA UCHUMI - KIGAILE

0:00 --:--

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Wananchi wa manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga hususan vijana na wanawake wanaojishughilisha na ujasiliamali wametakiwa kutumia ujio wa mbio za mwenge kwenye manispaa hiyo ili kukuza Uchumi wao.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Mbio za Mwenge Manispaa ya Kahama, Sadick Kigaile wakati akizungumza na Jambo Fm ofisi kwake kuhusu maandalizi ya ujio wa mwenge manispaa ya Kahama.

Sadick Kigaile.

“Siku ya mwenge tunapata simu mbalimbali sasa msisubiri siku ya mwenge njoo sasa tukupangie eneo ufanye biashara wakati wa mwenge,na maeneo haya tunatoa bure sasa vijana na wanawake na watu wengine njooni tuwape maeneo mfanye biashara siku ya mwenge ni siku ya kukuza Uchumi,” amesema Kigaile.

Kigaile ameongeza kuwa manispaa ya Kahama itapokea mwenge wa uhuru Agosti 21 ukitokea Shinyaga vijijini na utapokelewa katika kata ya Kagongwa na baada ya hapo utazindua na kukagua miradi mbalimbali kisha utakesha katika viwanja vya shule ya Sekondari Kishimba iliyopo mtaa wa Igomelo Masaki kata ya Malunga.

“Tunataraji kuupokea mwenge wa uhuru Agosti 21 katika kata ya Kagongwa kisha utakagua miradi mbalimbali ikiwemo miradi binafsi na miradi ya serikali,baada ya hapo Mwenge wa Uhuru utakesha eneo la Kishimba kwenye uwanja wa mpira,kwahiyo watu wa Manzese na Busoka mwenge umekuja kwenu hivyo jitokezeni kuulaki.” Ameongeza Kigaile.

Nao baadhi ya wananchi wa Kahama ambao ni wajasiliamali akiwemo Irene Mtui na Onesmo Zacharia wameishukuru halmashauri ya manispaa ya Kahama kwa kuwapa fursa hiyo kwenye mwenge wa uhuru na kutoa ombi kwa wanaogawa maeneo kutogawa maeneo mara mbili ili kuondoa sintofahamu baina ya wajasiliamali.

“Tunaishukuru manispaa yetu ya Kahama kwa kutupa fursa hii ya kufanya biashara hakika hii ni fursa itakayotuinua kiuchumi wajasiliamali wote wa Kahama,Ombi letu kwa wahusika wanaogawa maeneo ya biashara wasigawe maeneo mara mbili, ili kutoa sintofahamu baina ya wajasiliamali,” amesema Bi Mtui na Zacharia wajasiliamali wa Manispaa ya Kahama.

Katika wilaya ya Kahama Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri tatu za Kahama Manispaa,Ushetu na Msalala huku mwaka huu kauli mbiu ikiwa ni "Tanzania yetu sote, tushirikiane kwa Pamoja kuleta maendeleo."

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.