Skip to main content

TUMEPELEKA ZAIDI YA VIJANA 7,000 KUFANYA KAZI NJE - RAIS DKT. SAMIA

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake imeshapeleka vijana zaidi ya 7,000 kufanya kazi nje ya nchi, akisisitiza haki na stahiki zao zikasimamiwe vema.

TUMEPELEKA ZAIDI YA VIJANA 7,000 KUFANYA KAZI NJE - RAIS DKT. SAMIA
Studio Narration JAMBO FM

TUMEPELEKA ZAIDI YA VIJANA 7,000 KUFANYA KAZI NJE - RAIS DKT...

0:00 --:--

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake imeshapeleka vijana zaidi ya 7,000 kufanya kazi nje ya nchi, akisisitiza haki na stahiki zao zikasimamiwe vema.

Mkuu huyo wa nchi, amemwagiza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Uhusiano, Dk Everlyne Munisi, kwa kushirikiana na wenzake alitimize hilo.

Dkt Samia ameyasema hayo Ikulu jijini Dodoma leo, Jumatano Mei 6, 2026 alipozungumza baada ya kuwaapisha viongozi kadhaa aliowateua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni, katika hafla iliyofanyika leo Mei 6, 2026 Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

Amesema Serikali yake ilishaanza kutafuta ajira za vijana nje ya nchi, kwa muda mrefu zilikuwa zinapatikana nafasi lakini ndani ya wizara kulikuwa na tatizo.

“Mwaka huu tumeanza kufungua, tumeshapeleka zaidi ya vijana 7,000 nje, wasimamiwe haki, mawakala wasimamiwe, haki zao kule na sheria za kazi, Serikali za kule zifuate sheria zao, lakini na vijana wetu waende wakafuate sheria za watu na stahiki za vijana wetu zikapatikane,” amesema.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.