Skip to main content

TUMEBAINI KASORO MBALIMBALI DAWA ZA TIBA ASILI ZILIZOPO SOKONI - PROF. OTIENO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

TUMEBAINI KASORO MBALIMBALI DAWA ZA TIBA ASILI ZILIZOPO SOKONI - PROF. OTIENO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Baraza la Tiba asili na Tiba Mbadala limebainisha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, lilifanya zoezi maalum la ufuatiliaji wa dawa za tiba asili zilizopo sokoni (Post Market Surveillance) katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam ambapo katika zoezi hilo baadhi ya dawa zilibainika kuwa na mapungufu katika vifungashio, taarifa za lebo, ujazo, dozi na muda wa matumizi.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya Habari leo Juni 6, 2026 Jijini Dodoma Mwenyekiti Baraza hilo Prof. Nicolao Otieno amesema moja kati ya dawa hizo ni Joy ambayo ilibainika kuwa na sumu kuvu kwa kiwango kisichokubalika, hali iliyoashiria kutokuzingatiwa kwa viwango bora vya uzalishaji wa dawa asili hususan wakati wa ukaushaji na uhifadhi wa dawa ghafi na dawa zilizokamilika. 

"Kama inavyofahamika, sumu kuvu ni hatari kwa afya ya binadamu na inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo saratani ya ini, uharibifu wa figo, kupungua kwa kinga ya mwili pamoja na madhara mengine ya muda mrefu,"amesema.

Mwenyekiti Baraza hilo Prof. Nicolao Otieno.

Amesema dawa mbili za asili zilibainika kuwa zimechanganywa na kemikali  za dawa za kisasa zisizoruhusiwa ambazo hazikuainishwa kwenye lebo wala wakati wa usajili na kuongeza kuwa uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa baadhi ya dawa za tiba asili zimechakachuliwa kwa kuongezewa dawa za kisasa kinyume cha sheria. Hali hii ni hatari kwa afya ya jamii na ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na sheria zinazosimamia huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.

Aidha, Prof. Otieno ameongeza kuwa dawa nyingine zilizobainika kufanya hivyo pia ni Powaful Banana Medicine ambayo ilibadilishwa kuitwa Banana Medicine, inayotumika kama dawa ya kuongeza nguvu za kiume.

"Uchunguzi wa maabara umeonesha kuwa dawa hiyo imechanganywa na kemikali za dawa za kisasa za kuongeza nguvu za kiume ambazo ni Sildenafil na Tadalafil pamoja na dawa za maumivu aina ya Tramadol na Paracetamol, dawa hiyo imesajiliwa na Baraza na hutengenezwa na kampuni ya Powaful Products Company Ltd," ameongeza.

"Uchunguzi wa kimaabara haukubaini uwepo wa kemikali zozote zinazotokana na mimea," Prof.

Amesema dawa nyingine iliyobainika ni Vitamax (maarufu kama viasali), ambayo haijasajiliwa lakini imekuwa ikitumika katika jamii kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume, kwenye lebo yake imeonesha kuwa ina viambata vya miti dawa ambavyo ni Radix Eurycoma Longfolia, Radix Panax na Lepidium Meyenii. 

"Hata hivyo, uchunguzi wa kimaabara haukubaini uwepo wa kemikali zozote zinazotokana na mimea hiyo bali ulibaini uwepo wa kemikali za dawa za kisasa ambazo ni Sildenafil, Tadalafil, Tramadol na Paracetamol. Dawa hiyo hutengenezwa na kampuni ya Superfood International iliyopo nchini Malaysia," amesema.

Pia, amesema uwepo wa kemikali hizo za dawa za kisasa ndani ya dawa za tiba asili bila usimamizi wa kitaalamu unaweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji. Madhara hayo ni pamoja na matatizo ya moyo, figo na ini, shinikizo la damu, utegemezi wa dawa pamoja na hatari ya vifo kwa baadhi ya watumiaji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.