Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Rais Samia ameunda Tume hiyo ikiwa ni utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.

Tume hiyo inaundwa na Shabani Ally Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambqye ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume.
Walioteuliwa kuwa Makamishna wa Tume hiyo ni pamoja na (i) Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas (ii) Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Awadh Mohamed Bawazir na (iii) Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Aishieli Nelson Sumari.

Discussion
Reader comments
0 contributions