Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 nchini, imeongezewa muda hadi Aprili 24, 2026, ili iweze kukamilisha kazi yake.
Sababu za kuongezewa muda huo, ni pamoja na kuiwezesha kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyopokelewa, kutoa fursa kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kufanyia kazi baadhi ya vielelezo vipya vilivyowasilishwa.

Tume hiyo, inayoongozwa na Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman ilianza kutekeleza majukumu yake Novemba 20, 2025 na kutarajiwa kukamilisha kazi yake ndani ya kipindi cha siku 90.
Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, Tume iliongezewa muda wa kukamilisha kazi na kutakiwa kuwasilisha Ripoti kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kabla au ifikapo April 3, 2026.
Discussion
Reader comments
0 contributions