Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, Jaji Mstaafu Shaban Ally Lila amesema Tume imeanza kazi rasmi ya kubaini Wahusika na chanzo cha matukio ya ghasia yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi huo.
Jaji Lila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam hii leo Agosti 24, 2026 na kuongeza kuwa Tume hiyo itachunguza matukio ya ghasia, uvunjifu wa amani, ukiukwaji wa sheria pamoja na madhara yaliyotokea, huku ikilenga kubaini Wahusika na sababu zilizopelekea kutokea kwa matukio hayo.

Amesema Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ulifanyika kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini katika baadhi ya maeneo kulitokea ghasia na uvunjifu wa amani ambao ulisababisha madhara mbalimbali.
Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mstaafu Shaban Ally Lila na inasaidiwa na Makamishna sita, akiwemo Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.
Discussion
Reader comments
0 contributions