Skip to main content

TUHUMA: KABILA ANATAKA KUMPINDUA TSHISEKEDI - MUYAYA

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemtuhumu Rais Mstaafu Taifa hilo, Joseph Kabila kwa jaribio la kutaka kufanya mapinduzi, ili kurejea madarakani.

TUHUMA: KABILA ANATAKA KUMPINDUA TSHISEKEDI - MUYAYA
Studio Narration JAMBO FM

TUHUMA: KABILA ANATAKA KUMPINDUA TSHISEKEDI - MUYAYA

0:00 --:--

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemtuhumu Rais Mstaafu Taifa hilo, Joseph Kabila kwa jaribio la kutaka kufanya mapinduzi, ili kurejea madarakani.

Kupitia kauli ya Msemaji wa Serikali ya DRC, Patrick Muyaya amesema, uamuzi wa Kabila wa kutumia nguvu na silaha, unaashiria nia yake ya kutaka kukiuka Katiba.

Hivi karibuni, Serikali ya DRC ilisitisha shughuli za chama cha kisiasa cha Joseph Kabila cha (PPRD), kutaifisha mali zake na kumtuhumu kwa makosa ya usaliti wa nchi na uhalifu wa kivita, kutokana na hatua yake ya kuungana rasmi na waasi wa M23.

Mapema Oktoba 2026, Rais huyo wa zamani alitangaza kuongoza muungano mpya wa kisiasa na kijeshi unaojulikana kama Front for the Refoundation of the Nation (FRN).

Muungano huu umelenga kuuondoa madarakani utawala wa Rais Félix Tshisekedi kwa kutumia nguvu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.