Skip to main content

TTB YAMPA KONGOLE CHONGOLO KUWAHISHA MBOLEA KWA WAKULIMA

Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Imeipongeza Serikali kupitia Waziri wa Kilimo Mh Daniel Chongoro kwa kuhakikisha wakulima wa Tumbaku wanapata Mbolea kwa wakati ili kujiandaa na Msimu wa Kilimo 2026/2027.

TTB YAMPA KONGOLE CHONGOLO KUWAHISHA MBOLEA KWA WAKULIMA
Studio Narration JAMBO FM

TTB YAMPA KONGOLE CHONGOLO KUWAHISHA MBOLEA KWA WAKULIMA

0:00 --:--

Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Imeipongeza Serikali kupitia Waziri wa Kilimo Mh Daniel Chongoro kwa kuhakikisha wakulima wa Tumbaku wanapata Mbolea kwa wakati ili kujiandaa na Msimu wa Kilimo 2026/2027.

Akitoa Pongezi hizo kwa niaba ya wakulima wa zao la Tumbaku na wadau wa zao hilo  mkurungenzi wa bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Stanley Mnozya amesema kuwa wanaishukuru serikali kupitia wizara ya kilimo kwa kuhakikisha wanawapambania wakulima kupata Mbolea ya kupandia na kukuzia.

“Bodi ya Tumbaku Tanzanai kwa niaba ya wadau wa zao hili na wakulima kwa ujumla,tunatoa pongezi kwa serikali yetu ya awamu a sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wa kilimo Mh Daniel Chongoro kwa juhudi kubwa ya kuhahakisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati hadi hivi sasa mbolea ya kupandia na kukuzia tayari zimeshafika kwa wakulima hakika Waziri wetu wa kilimo amepambana licha kuwa kulikuwa na mikwamo ya hapa na pale hususan katika njia za kupitisha mbolea ila hatimaye mbolea ipo gharani kwa wakulima” Amesema Mnozya.

Sambamba na hilo Mnozya ameeleza kuhusu Bei ya Mbolea ambayo bado haijatoka na kufafanua kuwa bei ya Mbolea Ipo na kwamba Mh Waziri anatafuta njia kuhakikisha bei ya Mbolea inashuka ili iweze kuleta matunda kwa Mkulima.

“Najua mbolea imeshafika na wakulima wameziona ila wanajiuliza bei yake ikoje,ni kweli bei ya mbolea haijatoka ila ipo kitu kinachomnyima usingizi Waziri wetu wa kilimo Mh Chongoro ni namna ya kushusha bei ya mbolea ili isimuumize mkulima,kwasasa anafanya jitihada za kukutana na wadau wa zo hili yakiwemo mabenki ili kuona bei ya mbolea inapunguaje ili mkulima apate faida,niwatoe hofu wakulima Waziri wetu halali yupo kazini kuhakikisha mkulima ananufaika na kilimo chake hivyo bei ya mbolea muda si mrefu itatangazwa baad ya jitihada za Mh Waziri wetu kukamilika” Ameongeza Mnozya.

Katika hatua nyingine Mnozya ametoa wito kwa vyama vyote vya Msingi kutogawa Mbolea zilizoganga kwa wakulima na badala yake sitengwe ili ziweze kurudi kiwandani na wakulima wapewe mbolea Mpya.

“Kuna taarifa kutoka vyama mbalimbali nchini kupokea mbolea ambayo imeganda,tumewasiliana na msambazaji na ametupa ushirikiano mzuri Pamoja na TSJ na amesema ni kweli mbolea hizo zimeganda kutokana na mazingira ya kuhifadhi kule Mbeya ambako kuna baridi sana na amesema wakulima wasizitumie mbolea hizo atakuja kuzichukua na kuzirudisha kiwandani,hivya niwaombe vyama vya msingi vyote msigawe mbolea zilizoganda kwa wakulima bali ziwekeni pembeni na wataletewa mbolea mpya”Amesisitiza Mnozya.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushrika (KACU) Emmanuel Nyambi,Makamu mwenyekiti wa chama hicho Amocy Ntemi amesema kuwa wakulima wakitumia mbolea hiyo inaweza isilete matokeo Chanya kwenye zao hilo na kuwataka viongozi wa vyama vya msingi kufuata maelekezo ya wataalamu ikiwa ni Pamoja na kutogawa mbolea hizo ambazo zimeganda na kuzingatia maelekezo ya kujikinga na mvua za El-nino.

“Kwakweli tumejionea hizi mbolea ni kweli zimeganda na haziwezi kuleta tija kwa wakulima sasa niwaombe viongozi kuzingatia maagizo ya wataalamu kuhusu hizo mbolea,na niwaombe sana maelekeo ya mvua za Eli-Nino myafuate ili tupate tumbaku yenye tija” Amesema Ntemi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.