Skip to main content

TTB: WAKULIMA WA TUMBAKU NENDENI SHAMBANI MSIKATE TAMAA

Bodi ya tumbaku Tanzania (TTB) imewataka wakulima wa Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Kahama kuendelea na kilimo hicho bila kukata tamaa kwani msimu ujao wa 2026/2027 kuna neema kubwa katika zao hilo.

TTB: WAKULIMA WA TUMBAKU NENDENI SHAMBANI MSIKATE TAMAA
Studio Narration JAMBO FM

TTB: WAKULIMA WA TUMBAKU NENDENI SHAMBANI MSIKATE TAMAA

0:00 --:--

Bodi ya tumbaku Tanzania (TTB) imewataka wakulima wa Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Kahama kuendelea na kilimo hicho bila kukata tamaa kwani msimu ujao wa 2026/2027 kuna neema kubwa katika zao hilo.

Wito huo umetolewa na meneja wa bodi ya Tumbaku mkoa wa kitumbaku Kahama,Lucas Mihambo wakati akizungumza na vyama vya msingi katika kata zaUyogo na Bukomela.

Mihambo amesema kuwa msimu uliopita wa mwaka 2025/2026 zao la Tumbaku lilikuwa na changamoto nyingi ikiwemo kushuka kwa bei na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Wakulima turudi shambani tukalime kwa nguvu zote kwani msimu ujao ni msimu wenye neema kubwa kwani madaraja ya Tumbaku yameongezeka na wastani wa bei umepanda"Amesema Mihambo.

Sambamba na hayo Mihambo ameongeza kwa kuwataka wakulima kuhakikisha wanafuata taratibu zote za ulimaji wa zao la Tumbaku ikiwemo upandaji wa Tumbaku pamoja kutunza mbegu walizosia.

"Licha ya kuwepo kwa neema katika msimu ujao niwaombe sana wakulima tumieni kanuni bora za kilimo cha Tumbaku ili mzalishe tumbaku yenye ubora kuaanzia uandaaji wa mashamba hadi utunzaji wa mbegu mlizosia kwenye vitalu"

Katika hatua nyingine Mihambo amewatahadharisha wakulima Kuhusu mvua za El Nino zinazotarajia kunyesha huku akiwataka kuzingatia aina ya ulimaji na namna ya kutunza zao hilo.

"Kingine ndugu zangu niwaombe mchukue tahadhari juu ya mvua hizi za El nino,nendeni mkalime kwenye maeneo yenye miinuko yanayoweza kutiririsha maji lakini pia wekeni mifereji ya kupitiisha maji kwenye mashamba yenu huku mkiimarisha mabani yenu lakini pia tunzeni chakula kwa ajili ya familia zetu" Amesisìtiza Mihambo.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Simon Ntemi amesisitiza kuhusu usimamizi mzuri wa pembejeo huku akihaidi kufikisha pembejeo mapema ili kuwahi mvua za El Nino huku akikemea tabia ya baadhi ya wakulima kuuza pembejeo.

“Sisi Chama kikuu cha Ushirika KACU tunahaidi usimamizi mzuri wa pembejeo kulingana na mahitaji kwa kila chama cha msingi,tutahakikisha tunafikisha pembejeo mapema kwa wakulima ili kuwahi mvua za El-nino kwani tunatambua maeneo mengine ni vigumu kufikika wakati wa masika” Amesema Ntemi.

Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Katika mkoa wa kitumbaku Kahama kwa kushirikiana na wadau wa zao hilo wapo katika ziara ya kutembelea vyama vya msingi vya Tumbaku ili kutoa hamasa ya kilimo hicho na kueleza hatu za kuchukua dhidi ya mvua za El Nino.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.