Skip to main content

TRUMP AZUA UTATA SITISHO MASHAMBULIZI YA NISHATI URUSI, UKRAINE

Rais wa Marekani, Donald J.Trump, ametoa tangazo la ghafla la kusitisha mashambulizi dhidi ya malengo ya miundombinu ya nishati kati ya Urusi na Ukraine, akieleza kuanza kufanyiwa kazi kwa tangazo hilo mara moja.

TRUMP AZUA UTATA SITISHO MASHAMBULIZI YA NISHATI URUSI, UKRAINE
Studio Narration JAMBO FM

TRUMP AZUA UTATA SITISHO MASHAMBULIZI YA NISHATI URUSI, UKRA...

0:00 --:--


Rais wa Marekani, Donald J.Trump, ametoa tangazo la ghafla la kusitisha mashambulizi dhidi ya malengo ya miundombinu ya nishati kati ya Urusi na Ukraine, akieleza kuanza kufanyiwa kazi kwa tangazo hilo mara moja.

Hata hivyo, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, ameeleza kuwa bado anasubiri kupata maelezo ya kina kuhusiana na tangazo la Trump na makubaliano hayo.

Hadi sasa, hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali ya Putin kuhusu tangazo hilo, ambalo linajiri baada ya siku kadhaa za shinikizo kubwa kutoka kwa Trump akitaka Ukraine isitishe mashambulio yake dhidi ya vituo vya kusafisha mafuta nchini Urusi.

Trump anayashtumu mashambulio hayo kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta ya dizeli, hali inayokiweka katika wakati mgumu Chama chake cha Republican kuelekea uchaguzi wa katikati ya muhula (midterms) mwezi ujao.

Siku ya Jumamosi, uhusiano kati ya viongozi hao wawili ulizorota zaidi baada ya Trump kumwonya Zelenskiy kwa kusema anapaswa "kusitisha mara moja" mashambulio hayo, huku akiwashauri Raia wa Ukraine kumchagua kiongozi mwingine katika uchaguzi mpya, akidai Zelenskiy amekosa fursa kadhaa za kufikia makubaliano na Urusi.

"Anza kufanya kazi mara moja, kuna kusitishwa kwa mashambulio ya nishati katika Vita kati ya Urusi na Ukraine. Pande zote mbili zimekubaliana. Msikiuke!" Donald Trump

Kulingana na chanzo kilichokaribu mzozo huo kwa sharti la kutobainishwa jina amesema, Marekani ilitishia kusitisha utoaji wa taarifa za kijasusi kwa Ukraine pamoja na ununuzi wa silaha kupitia mfumo wa Prioritised Ukraine Requirements List (PURL), ikiwa ni mbinu ya kuishinikiza Kyiv kuacha kushambulia vituo vya nishati vya Urusi.

Mtu huyo aliongeza kuwa Rais Zelenskiy kwa sasa yupo kwenye mashauriano na viongozi wa Ulaya ili kutafuta njia ya kutuliza mtekamo wa mambo na uhusiano wao na Trump.

Hata hivyo Rais Zelenskiy alithibitisha kuwa tayari amejadili tangazo hilo la Trump na Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, pamoja na Rais wa Finland, Alexander Stubb.

Kadharika hadi sasa Ikulu ya Marekani (White House) haijatoa majibu ya haraka kufuatia maombi ya kutoa ufafanuzi kuhusu swala hilo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.