Skip to main content

TRILIONI 1.9 KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO SHINYANGA

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

TRILIONI 1.9 KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO SHINYANGA

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba, 2025 hadi Juni 2026 katika kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) ya mkoa wa Shinyanga inayoongozwa na mwenyekiti wa cham hicho Mabala Mlolwa.

Akisoma taarifa hiyo RC Mhita   amesema kwa kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya sita mkoa wa Shinyanga umepokea Trilioni 1.9 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo,ambapo miradi kadhaa imetekelezeka kupitia fedha hizo  na kwamba wananchi wa mkoa huo wameshuhudia maendeleo ya haraka katika katika sekta ya kilimo, mifugo, madini, viwanda , biashara, pamoja na huduma za jamii, Afya, Elimu, Nishati na Maji.

Akizungumzia hali ya uongozi katika mkoa huo RC Mhita ametoa shukrani kwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan kwa kumteua mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi kuwa waziri wa mambo ya ndani na mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba kuwa naibu waziri wa nishati

Akielezea  pia kuhushu hali ya uchumi wa mkoa wa Shinyanga RC Mhita  Amesema, mkoa huo  unaendelea kuimarika kiuchumi  ambapo pato halisi limeongezeka kutoka sh. bilioni 7.5 mwaka 2021 hadi sh.bilioni 9.2 mwaka 2026 sawa na ukuaji wa asilimia 22. Na kwamba pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka sh. Milioni 1.8 mwaka 2021 hadi Sh.milioni 1.9 mwaka 2026 sawa na ongezeko la asilimia 7.

Kuhusu sekta ya afya RC Mhita Mhita amesema serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya katika mkoa huo baada ya kupokea jumla ya shilingi   bilioni 99.0 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kukamilisha  hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo iliyopo  katika kata ya Mwawaza, kwa kujenga majengo ya EMD, OPD, Jengo la utawala, Jengo la Uraibu wa Madawa ya kulevya na kituo cha tiba jumuishi, kununua vifaa tiba, ujenzi wa nyumba za watumishi pamoja na kuongezeka kwa madawa na vitendanishi.

Kwa upande wa elimu RC Mhita amesema mkoa huo umepokea jumla ya shilingi bilioni 205.2  kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu pamoja na utekeleaji wa miradi mbalimbali ili kuinua ubora katika ngazi zote mkoani humo.

RC Mhita pia amezugumzia hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa huo kwa kuanisha kwamba  mkoa huo umepokea shilingi  bilioni 163.3 ili kuhakikisha kaya nyingi zinaunganishwa na huduma ya maji, na kwamba upatikanaji wa maji kwa wananchi kwa sasa ni asilimia 79 kutoka 63 kwa maeneo ya mijini na vijijini asilimia 68 kutoka 51.

RC Mhita pia amezungumzia sekta ya kilimo katika mkoa huo kwa kuanisha kuwa serikali imeendelea na ujenzi  wa Skimu za bwawa la Nyida na Melenge,ili  kuimarisha huduma za ugani kwa kununua vitendea kazi ikiwamo Pikipiki, vipima udongo na vishikwambi.

Lakini pia RC Mhita ameizungumzia sekta ya mifugo kwa kusema kuwa serikali imeongeza usambazaji wa dawa  za ruzuku za kuogeshea mifugo, kuimarisha huduma ugani kwa kugawa pikipiki 534 kwa ajili ya maafisa mifugo, pamoja na kuongeza minada ya mifugo kutoka 25 hadi 30.

Kuhusu sekta ya madini  RC Mhita amesema  serikali imeendelea kuwathamini wachimbaji wadogo katika kukuza mtaji yao na kwamba kumekuwa na ongezeko la utoaji wa leseni kwa chimbaji wadogo kutoka 332 hadi 1766.

Kwa upande wa miundombinu amesema kumekuwa na ongezeko la mtandao wa barabara za lami kwa kilomita 57 ,barabara za changarawe kilomita 454, na kukamilika kwa ujenzi wa madaraja 18 ,makaravati 2,113, na pamoja na kuendelea kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kahama- Bulyanhulu kilomita 73 kwa gharama ya sh.bilioni 100.6 na ujenzi umefikia asilimia 78.21.

Aidha kuhusu nishati RC Mhita amesema  serikali ya awamu ya sita  imetoa jumla ya  shilingi  bilioni 426 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini, pamoja kuendelea kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme jua katika kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu kwa kuzalisha Megawati 100 kwa awamu ya pili.

Kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi amesema kumekuwa na ongezeko la  utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo kiasi cha shilingi  bilioni 11.3 zimetolewa kwa vikundi 941 vya wanawake, Vijana 599 na watu wenye ulemavu vikundi 110.

Kwa upande wa usaidiaji wa kaya masikini kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF RC Mhita amesema serikali imetoa shilingi   bilioni 59.5 kwa walengwa elfu 35,055 kutekeleza miradi 77 ya miundombinu ya elimu, afya, barabara, pamoja na kuwezesha walengwa elfu 15,103 kujiongezea kipato kupitia ufugaji na kilimo.

Kuhusu utawala bora mkoa umepokea shilingi  bilioni 22,2 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala na nyumba za watumishi, katika Hamashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga DC, Ushetu na ujenzi wa Jengo la Ofisi ya mwendesha Mashtaka.

Kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi unaofanywa na serikali ambapo  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amempongeza   Mkuu huyo wa mkoa kwa usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuitendelea haki ilani ya uchaguzi ya Chama hicho.

Mkoa wa  Shinyanga una ukubwa wa kilomita za mraba elfu 18,557 na unajumla ya watu milioni 2,2 wanaume wakiwa milioni 1.102 na wanawake milioni 1.13 kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.