Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Singida, imekabidhi vifaa vya usafi kwa wafanyabiashara wa Soko la Msufini ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usafi na utunzaji wa mazingira ndani ya Manispaa ya Singida.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa wakati Manispaa ya Singida ikiendelea na zoezi la usafi katika soko hilo kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa wafanyabiashara na wananchi wanaotumia soko hilo.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni mapipa ya taka (dustbins), mifagio na chepe, ambavyo vitasaidia wafanyabiashara kuendelea kutunza usafi wa soko na kuhakikisha taka zinakusanywa na kutupwa katika maeneo yanayostahili.
Katika hatua nyingine, zoezi la usafi limeendelea katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Singida, ambapo wakazi wa Kata ya Minga nao wameungana katika kufanya usafi na kuzibua mitaro ili kuhakikisha maji ya mvua yanapita vizuri.
Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi endelevu ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño, hususan mafuriko yanayoweza kutokea kutokana na kuziba kwa mitaro na mifereji ya maji.
Manispaa ya Singida inaendelea kuhamasisha wananchi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali kushiriki katika shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira kwa pamoja ili kuweka maeneo yao katika hali ya usafi na usalama.
Discussion
Reader comments
0 contributions