Skip to main content

TRA SHINYANGA YAANZISHA OFISI INAYOTEMBEA

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

TRA SHINYANGA YAANZISHA OFISI INAYOTEMBEA

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  mkoa wa Shinyanga imeanza rasmi kutoa huduma za ofisi inayotembea ili kuwafikia wateja katika maeneo yao, lengo likiwa ni kupunguza adha ya wateja wao  kutembea  umbali murefu  kufata huduma pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Akizungumzia huduma afisa wa kodi TRA mkoa wa Shinyanga Semeni Mbeshi amesema ofisi hiyo imeanza kutoa huduma  katika mnada wa Tinde ulipo halimashauri ya wilaya ya Shinyangana kwamba gari hilo litatoa huduma kwa muda wa siku tatu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga.

“Kama mnavyoona gari letu hilo linapita katika maeneo tofauti kumfikia mlipa kodi asipate tabu na leo tumeanza na Tinde lakini tunarajia kuyafikia maeneo ya Mwakitolyo,Didia na Mhunze wilayani Kishapu”amesema Mbeshi  

Nao baadhi ya wafanyabiashara waliofikiwa na huduma hiyo katika eneo la Tinde wameishukuru TRA kwa kuwafikia katika maeneo yao na  kuaninisha kwamba sasa mamlaka hiyo imetengeneza mazingira rafiki ya ulipaji wa kodi wa hiari maana hapo awali iliwabidi kutembea kuzifata ofisi za TRA   na wakati mwingine kufunga biashara zao. 

Kupitia ubunifu huo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia  kuwafikia wananchi na kusogeza    huduma za kodi karibu zaidi na walipakodi. Kupitia ofisi hiyo, wananchi watapata  huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa namba ya mlipakodi (TIN), elimu ya kodi, ushauri kuhusu masuala ya kodi pamoja na utatuzi wa changamoto zinazohusiana na huduma za TRA.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.