Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kanda ya kati inayoundwa na mikoa ya Shinyanga, Tabora, Katavi, Singida, Kigoma, Dodoma na mkoa wa kikodi Kahama wametembelea kiwanda cha Jambo foodi product cha mjini Shinyanga, ili kutoa shukrani kwa ulipaji kodi wa ufasaha, pamoja na kuboresha mahusiano kwa kusikiliza changamoto za kikodi zinazowakabili, ili kuzitatua.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho, Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga, Emanuel Maro ameshukuru uongozi wa kampuni ya jambo kuwaruhusu kutembelea kiwanda na kuangalia uzalishaji kwa imekuwa ni fursa nzuri kwa taasisi hiyo kuangalia fursa zinazoendelea kwa imekuwa ni nafasi kwa mameneja wa taasisi hiyo kwa kanda ya ziwa kujifunza,

Maro amesema licha ya kushirikiana na kampuni hiyo katika masuala ya kodi, lakini kwa sasa wametambua uhalisia, huku akiahaidi kuendelea kutatua changamoto zitakazokuwa zinajitokeza katika huduma, ili ulipaji wa kodi uweze kufanyika kwa wepesi.
Kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, ukanda wa kati kwa niaba ya Mameneja wa Mikoa, Maro amesema mwaka wa fedha 2025/2026 mikoa hiyo imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya asilimi l00 kwa miezi 12 ya makusanyo.
Amesema, pia wameadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza tarehe 5 hadi tarehe 9 october 2026 kwa kutoa zawadi kwa walipa na kuendelea kuwashukuru kwa uliapji kodi huku akihaidi kuendelea kutoa ushirikiano.

MKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA JAMBO GROUP KHAMIS SALUM KHAMIS AKIWATEMBEZA MAMENEJA WA TRA KANDA YA KATI KUAGALIA UZALISHAJIKATIKA KIWANDA HICHO
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jambo Food Product, Khamis Salum Khamis amehaidi kutoa ushirikiano kwa TRA, ili kuchochea maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.

MENEJA WA TRA KITENGO CHA HUDUMA KWA MLIPA KODI MKOA WA SHINYANGA RAMADHANI SENGO
Akizungumzia wiki ya huduma kwa wateja,Meneja kitengo huduma kwa mlipa kodi, Ramadhani Sengo amesema taaisisi hiyo imekutana na walipa kodi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa walipa kodi.
Sengo amesema, katika kuthamini mchango wa wawalipa kodi katika kuchochea maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)mkoa wa Shinyanga itaendelea kuboresha huduma hususan katika maeneo ambayo yameonekana na mapungufu kwa upande wa TRA.

TRA inaendela kuwahimiza wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ya kugharamia miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.
Aidha, mamlaka hiyo imekuwa ikisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti pale zinapohitajika na kuhakikisha wanatoa risiti kwa wateja wao ili kusaidia kuongeza uwazi na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

TRA inawataka wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa sheria za kodi na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa maendeleo ya taifa.

Discussion
Reader comments
0 contributions