Skip to main content

TNCC KUINUA MITAJI, UJUZI YA WAFANYABIASHARA KIGOMA

Wafanyabiashara Mkoani Kigoma, wamehimizwa kujiunga na Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) ili kuongeza mitaji, kupanua shughuli zao na kunufaika na fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana ndani na nje ya nchi.

TNCC KUINUA MITAJI, UJUZI YA WAFANYABIASHARA KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

TNCC KUINUA MITAJI, UJUZI YA WAFANYABIASHARA KIGOMA

0:00 --:--

Wafanyabiashara Mkoani Kigoma, wamehimizwa kujiunga na Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) ili kuongeza mitaji, kupanua shughuli zao na kunufaika na fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana ndani na nje ya nchi.

Rai hiyo. imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, katika Kikao cha Kimkakati cha Wadau wa biashara kilichoratibiwa na Ofisi ya TNCC Mkoa wa Kigoma, kwa lengo la kujadili mikakati ya kukuza biashara na kuimarisha uchumi wa wananchi.

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara, (Picha na Tryphone Odace.)

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Chuachua amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ili kurahisisha shughuli za kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kufungua fursa zaidi kwa wafanyabiashara.

Aidha alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa biashara na maendeleo ya uchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) Mkoa wa Kigoma, Obadia Kabuga alisema kikao hicho kimewakutanisha mashirika na wadau mbalimbali wa biashara kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na kuweka mikakati ya kuwawezesha kukuza shughuli zao kiuchumi.

Baadhi ya wafanyabiashara Mjini Kigoma wakiwa katika kikao cha TNCC, (Picha na Tryphone Odace)

Kabuga alieleza kuwa ushiriki wa wadau katika majukwaa hayo ni muhimu katika kubadilishana uzoefu, kupata elimu ya biashara na kubaini fursa zinazoweza kuwasaidia wafanyabiashara kuongeza tija na kupanua mitaji yao.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata, wakisema itawasaidia kuboresha usimamizi wa biashara zao, kufanya maamuzi sahihi na kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuongeza kipato.

Baadhi ya wafanyabiashara Mjini Kigoma wakiwa katika kikao cha TNCC, (Picha na Tryphone Odace)

Walisema elimu hiyo ni muhimu kwa wafanyabiashara, hususan katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kuzuia ukuaji wa biashara zao.

Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) ni taasisi inayolenga kuwakutanisha wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi pamoja na Serikali, ili kuimarisha mazingira ya biashara, kuhamasisha uwekezaji na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.