Skip to main content

TMDA YAKAMATA DAWA BANDIA KIGOMA

Wananchi Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kuwapatia elimu ya kutambua dawa bandia na zisizofaa kwa matumizi ya wanadamu na wanyama zinazouzwa kwenye maduka ya dawa muhimu za binadamu na mifugo ili kulinda afya zao.

TMDA YAKAMATA DAWA BANDIA KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

TMDA YAKAMATA DAWA BANDIA KIGOMA

0:00 --:--

Wananchi Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kuwapatia elimu ya kutambua dawa bandia na zisizofaa kwa matumizi ya wanadamu na wanyama zinazouzwa kwenye maduka ya dawa muhimu za binadamu na mifugo ili kulinda afya zao.

Wakizungumza mara baada ya mkutano wa wanahabari na meneja wa TMDA kanda ya magharibi, wananchi hao wamesema taasis hiyo inapaswa kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii na mikutano ili kutoa elimu ya utambuzi wa dawa.

Miongonimwa wananchi hao ni Richard Gaspa mkazi wa Kibirizi na Irene Abeli mkazi wa Airport wmekiri kutokuwa na uelewa wa namna ya kutambua dawa bandia na kuwa hali hiyo inaweza kuhatarisha maisha ya wananchi wengi endapo hawatapatiwa elimu.

Kwa upande wake Meneja wa TMDA kanda ya Magharibi Christopher Migoha amesema wamefanikiwa kukamata dawa na kuziondoa sokoni zenye thamani ya zaidi ya shilingi million 5 na nusu katika wilaya ya kigoma na Kasulu.

Hata hivyo amewataka wananchi kuhakikisha wananunua dawa kwenye maduka ya dawa muhimu kulingana na maelezo ya daktari ili kupunguza usugu wa dawa huku akiwataka pia watoa huduma kutoa huduma kwa wananchi kulingana na taratibu na sheria zilizowekwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.