Skip to main content

TFRA, ZASCO ZASAINI MKATABA UZALISHAJI MBOLEA YA MWANI

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na Kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO) zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano itakayowezesha uzalishaji wa mbolea ya mwani, hatua inayolenga kuongeza thamani ya zao hilo na kuimarisha sekta ya kilimo.

Makubaliano hayo yalisainiwa wakati wa Kongamano la Uchumi wa Buluu ambalo ni moja ya matukio katika Tamasha la Kizimkazi, lililokusanya wadau mbalimbali wa uvuvi kujadili fursa za maendeleo zinazotokana na rasilimali za bahari.

Mtendaji Mkuu wa ZASCO, Dk Masoud Rashid Masoud, amesema utekelezaji wa ushirikiano huo utaanza mara baada ya kukamilika kwa kiwanda cha kuchakata mwani kinachojengwa na Serikali ya Zanzibar na kinachotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Amesema kiwanda hicho kitazalisha bidhaa mbalimbali zitokanazo na mwani, ikiwemo mbolea ya kimiminika, huku TFRA ikisimamia uthibitishaji wa ubora wake ili kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa kabla ya kuingia sokoni.

Mkurugenzi wa TFRA, Joel Laurent, amesema ushirikiano huo utasaidia kukuza kilimo chenye tija Zanzibar, akibainisha kuwa majaribio kwa wakulima na mashamba darasa yatafanyika ili kuhakikisha matumizi sahihi ya mbolea hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.