Rais Samia Suluhu Hassan, amesema matumizi ya teknolojia katika majengo ya Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, yanapaswa kuongeza tija, kurahisisha utoaji huduma na kupunguza urasimu katika kuhudumia wananchi.
Akizungumza leo, Oktoba 30, 2025, wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba, Rais Samia amesema wananchi hawapaswi kusafiri kutoka mikoa ya mbali kwenda Mtumba kufuatilia huduma zinazoweza kupatikana walipo, akitaja Rukwa, Kigoma na Mtwara.

“Mwananchi kutoka Rukwa, Kigoma, Mtwara asitumie muda na fedha nyingi kuja kufuatilia jambo lake ambalo lingeweza kushughulikiwa alipo,” amesema leo, Oktoba 30, 2026.
Amesisitiza mifumo ya TEHAMA katika taasisi za Serikali iunganishwe ili taarifa zinazopokelewa na kuchakatwa katika taasisi moja ziweze kusambazwa kwa urahisi kwenye taasisi nyingine.
Amesema teknolojia iliyowekwa Mtumba inapaswa kutumika kurahisisha kazi za Serikali na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa urahisi bila kukumbana na urasimu.
Discussion
Reader comments
0 contributions