Wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS Kanda ya Magharibi wametoa mafunzo ya kujenga uelewa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali yanayohusiana na usimamizi wa ubora wa chakula na vipodozi kwa Kamati ndogo ya Chakula na Vipodozi Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa kutoka TBS, Hamis Seleleko ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa kuwa kinara wa utekelezaji na usimamizi wa chakula na vipodozi pamoja na usajili wa majengo ya kuhifadhia bidhaa hizo.

Katika mafunzo hayo Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Marko Mayagule pamoja na kupitishwa katika miongozo na majukumu muhimu ya Kamati, wamehimizwa kufanya kazi kwa Ushirikiano na TBS, ili kufanikisha usimamizi wa chakula na vipodozi.
Mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni katika kutekeleza ushirikiano muhimu baina ya TBS na OWM - TAMISEMI, wa kuwatumia wataalamu waliopo katika Halmashauri kusimamia Sheria, Taratibu, kanuni na ubora wa chakula na vipodozi pamoja na mazingira yake.



Discussion
Reader comments
0 contributions