Skip to main content

TATHIMINI MADARAJA YA NYOTA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA INAENDELEA - WIZARA

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inaendelea kufanya Tathmini ya Madaraja ya Nyota (Star Rating Assessment) katika vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini.

TATHIMINI MADARAJA YA NYOTA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA INAENDELEA - WIZARA
Studio Narration JAMBO FM

TATHIMINI MADARAJA YA NYOTA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA...

0:00 --:--

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inaendelea kufanya Tathmini ya Madaraja ya Nyota (Star Rating Assessment) katika vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini.

Zoezi hilo, ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha ubora wa huduma za afya kwa wananchi, tathmini ambayo inayofanyika katika mikoa minane nchini ikiwemo Mkoa wa Lindi.

Wizara inalenga kupima na kupanga vituo vya kutolea huduma za afya katika madaraja ya nyota kulingana na viwango vya ubora wa huduma zinazotolewa, pamoja na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.

Aidha, zoezi hilo pia linachangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuimarisha mifumo ya afya, kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na zenye viwango vinavyokubalika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.