Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amethibitisha kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, ambaye amefariki dunia akiwa chini ya uangalizi wa madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kuhusu msiba huo, Chacha amesema Mkoa wa Tabora umepoteza kiongozi muhimu aliyekuwa akitekeleza majukumu yake kwa weledi, uadilifu na kujituma katika kuhakikisha usalama wa wananchi pamoja na mali zao unadumishwa wakati wote.
Ameeleza kuwa kifo cha SACP Abwao ni pigo kubwa kwa Jeshi la Polisi na wananchi wa Mkoa wa Tabora kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha amani, usalama na utulivu wa jamii.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi inaendelea na maandalizi ya shughuli za kuaga mwili wa marehemu pamoja na mazishi yake. Amesema ratiba rasmi ya shughuli hizo itatangazwa baadaye.
Wakati huo huo, viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi kutoka maeneo tofauti wameendelea kutuma salamu za pole na rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa pamoja na Jeshi la Polisi kufuatia msiba huo.
Kifo cha SACP Richard Abwao kimeacha simanzi kubwa miongoni mwa askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora na wananchi waliokuwa wakinufaika na utendaji wake katika kulinda amani na usalama wa jamii.
Discussion
Reader comments
0 contributions