Skip to main content

TANTRADE, WAZALISHAJI WA NDANI KUENDELEZA USHIRIKIANO UBORESHAJI WA BIDHAA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania – TanTrade imesema itaendelea kushirikiana na wazalishaji wa ndani kuboresha ubora na ushindani wa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, ili kuongeza thamani na kufungua masoko zaidi ndani na nje ya Tanzania.

TANTRADE, WAZALISHAJI WA NDANI KUENDELEZA USHIRIKIANO UBORESHAJI WA BIDHAA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania – TanTrade imesema itaendelea kushirikiana na wazalishaji wa ndani kuboresha ubora na ushindani wa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, ili kuongeza thamani na kufungua masoko zaidi ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa kufunga maonesho ya 33 ya Nanenane katika viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Ephraim Balozi Mafuru, amesema ushiriki wa mamlaka hiyo katika maonesho mbalimbali unalenga kuwafikia wazalishaji na kuwapatia taarifa kuhusu fursa za masoko, viwango vya ubora na namna ya kuongeza thamani ya bidhaa zao.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Ephraim Balozi Mafuru.

Mafuru amesema kupitia kampeni ya “Made in Tanzania”, TanTrade inalenga kuhakikisha bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini zinatambulika zaidi, zinafikia viwango vinavyohitajika na kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.

Amesema takwimu zinaonyesha Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nje zenye thamani ya takribani dola bilioni 10 za Marekani, huku TanTrade ikiamini kuwa kuna uwezo wa kuongeza thamani hiyo hadi zaidi ya dola bilioni 20.

Hata hivyo, amesema kufikia lengo hilo kunahitaji ushirikiano wa Serikali, sekta binafsi na wadau wengine, huku wazalishaji wakitakiwa kuelewa mahitaji ya masoko ya kimataifa na kuhakikisha bidhaa zao zinafikia viwango vinavyotakiwa.

Amesema TanTrade itaendelea kufanya tafiti za masoko kwa kubaini mahitaji ya walaji, kuelewa vigezo vya ubora vinavyohitajika, pamoja na kuchambua gharama zinazotumika katika mnyororo mzima wa thamani.

Mafuru amewataka wazalishaji wa bidhaa na watoa huduma nchini kutumia ofisi za TanTrade kupata elimu na taarifa kuhusu viwango vya ubora, gharama na mikakati bora ya kuingia katika masoko mbalimbali.

Kwa upande mwingine, amesema maonesho ya Nanenane yameendelea kuonyesha ongezeko la uzalishaji na biashara ya bidhaa zinazotengenezwa nchini, huku wazalishaji wakiongeza ubora na kuanza kufikia masoko ya kimataifa.

Maonesho hayo ya siku nane yamewakutanisha zaidi ya waoneshaji 1,300 kutoka katika sekta mbalimbali za uzalishaji na biashara, yakitoa fursa ya kutangaza bidhaa, kuhamasisha uwekezaji na kuwaunganisha wazalishaji na masoko.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.