Skip to main content

TANESCO YATAMBULISHA RASMI MFUMO WA 'SMART HOUSE'

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetambulisha rasmi mfumo mpya wa kufunga nyaya za umeme majumbani utakaowezesha wateja kufuatilia matumizi ya umeme kupitia simu ya mkononi, unaojulikana kama 'Smart House'.

TANESCO YATAMBULISHA RASMI MFUMO WA 'SMART HOUSE'

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetambulisha rasmi mfumo mpya wa kufunga nyaya za umeme majumbani utakaowezesha wateja kufuatilia matumizi ya umeme kupitia simu ya mkononi, unaojulikana kama 'Smart House'.

Mfumo huo umetambulishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, wakati akimweleza mambo muhimu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alipotembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Twange amesema kupitia mfumo huo, mteja ataweza kuona kifaa gani ndani ya nyumba kinatumia umeme mwingi na kukizima akiwa popote alipo kupitia simu yake.

“Hata kama uko Mwanza au Dubai na nyumba ipo Kigoma, unaweza kuzima kifaa hicho ukiwa huko, hivyo kudhibiti matumizi ya umeme usiyoyahitaji,” amesema.

Ameeleza kuwa ubunifu huo umetokana na malalamiko ya wateja waliokuwa wakidai kuwa matumizi yao si makubwa, lakini umeme unaisha kwa haraka.

Aidha, amesema baadhi ya wateja walikuwa wakilalamikia mita kutosoma vizuri na hivyo kulazimika kuiomba TANESCO kufanya ukaguzi na kuutaja Mfumo huo kusaidia kubaini kifaa kinachotumia umeme mwingi na kurahisisha ufuatiliaji wa matumizi.

"Teknolojia hii mpya inatarajiwa kuzinduliwa rasmi muda si mrefu kabla ya kusambazwa kwa wateja nchini, hatua inayoonyesha juhudi za wahandisi wa TANESCO katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili watumiaji wa umeme," amesema. 

Aidha, amewahimiza wateja kuendelea kutoa maoni na changamoto zao, akieleza kuwa shirika hilo linaendelea kubuni teknolojia na huduma mpya ili kuboresha huduma zake.

Kwa upande wa nishati safi ya kupikia, Twange amesema amemweleza Dkt. Mwinyi kuhusu hatua zinazochukuliwa kutekeleza mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati hiyo.

Amesema kwa sasa TANESCO inaendelea na mpango wa Bill Financing, unaowezesha wateja wapya na waliopo kukopeshwa majiko ya umeme na kurejesha gharama zake taratibu kupitia ununuzi wa umeme.

“Mpango huu umepata mwitikio mzuri na umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90. Ndiyo maana tumehusisha sekta binafsi kupitia mikataba mbalimbali ili kuongeza upatikanaji wa majiko kwa wananchi,” amesema.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.