Skip to main content

TANESCO YAFANYA UKAGUZI WA MITA ZA UMEME KALIUA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na zoezi la ukaguzi wa mita za umeme kwa wateja wake, likilenga kuhakikisha matumizi ya umeme yanafanyika kwa usahihi na kwa mujibu wa taratibu.

TANESCO YAFANYA UKAGUZI WA MITA ZA UMEME KALIUA
Studio Narration JAMBO FM

TANESCO YAFANYA UKAGUZI WA MITA ZA UMEME KALIUA

0:00 --:--

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na zoezi la ukaguzi wa mita za umeme kwa wateja wake, likilenga kuhakikisha matumizi ya umeme yanafanyika kwa usahihi na kwa mujibu wa taratibu.

Katika hatua hiyo, timu ya TANESCO Mkoa wa Tabora imefanya ukaguzi kwa baadhi ya wateja na wafanyabiashara katika Kata ya Kashishi, Wilaya ya Kaliua, Jimbo la Ulyankulu, ambapo hakukuwa na mteja aliyebainika kutumia umeme bila kufanya malipo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mhandisi Erasto Waya kutoka TANESCO Mkoa wa Tabora amesema matokeo hayo yanaonesha umuhimu wa elimu inayotolewa mara kwa mara kwa wateja kuhusu matumizi sahihi na halali ya huduma ya umeme.

Kwa mujibu wa Mhandisi Waya, ukaguzi huo ni sehemu ya kampeni endelevu inayotekelezwa katika wilaya zote saba za Mkoa wa Tabora, kwa lengo la kuhakikisha kila mteja anatumia umeme kupitia mita yake na kuzingatia taratibu za matumizi ya huduma hiyo.

Amesema TANESCO itaendelea na ukaguzi huo pamoja na kutoa elimu kwa wateja ili kuimarisha uelewa kuhusu matumizi salama na halali ya umeme.

Aidha, TANESCO imewataka wateja wanaokutana na changamoto katika huduma ya umeme kutumia namba 180, ambayo ni ya bure, ili kupata msaada na utatuzi wa changamoto zao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.