Skip to main content

TANESCO SINGIDA WAONGEZEWA ARI UBORESHAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

TANESCO SINGIDA WAONGEZEWA ARI UBORESHAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Singida wametakiwa kutunza na kutumia kwa ufanisi vyombo vipya vya usafiri walivyokabidhiwa, ili kuboresha huduma za umeme kwa wananchi Mkoani humo.

Hafla hiyo Mkuu imefanyika Uwanja wa Bombadia Mjini Singida na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema, umeme ni muhimili wa uchumi na maendeleo, akibainisha kuwa upatikanaji wake wa uhakika utachochea ukuaji wa viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi mkoani humo.

Amesisitiza kuwa magari hayo ni rasilimali ya umma inayopaswa kuthaminiwa, akiwataka watumishi wa TANESCO kuyatunza kwa uangalifu mkubwa sawa na mali zao binafsi ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Aidha, amesema upatikanaji wa umeme mkoani Singida utaendelea kuboreshwa, ili kufikia malengo ya maendeleo ya mwaka 2030 yanayolenga kuhakikisha kila kaya inapata huduma ya umeme.

Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida, Mhandisi Mwamvita Ally amesema, magari hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia nishati ya uhakika.

Ameeleza kuwa magari hayo manne yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 800 yanajumuisha magari mawili makubwa yenye crane zenye uwezo wa tani saba kwa ajili ya kunyanyua nguzo za umeme, pamoja na magari mawili madogo kwa matumizi ya kawaida, hatua itakayorahisisha utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo mkoani Singida.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.