Skip to main content

TANESCO KATAVI YAENDA 'EXTRA MILE' IKITOA VITI MWENDO KWA WATOTO WENYE MAHITAJI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Katavi, limefanya ziadaya jukumu lake la kusambaza umeme, baada ya kutoa viti mwendo saba vyenye thamani ya shilingi milioni 3.15 kwa watoto wenye mahitaji mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kurudisha kwa jamii.

TANESCO KATAVI YAENDA 'EXTRA MILE' IKITOA VITI MWENDO KWA WATOTO WENYE MAHITAJI
Studio Narration JAMBO FM

TANESCO KATAVI YAENDA 'EXTRA MILE' IKITOA VITI MWENDO KWA WA...

0:00 --:--

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Katavi, limefanya ziadaya jukumu lake la kusambaza umeme, baada ya kutoa viti mwendo saba vyenye thamani ya shilingi milioni 3.15 kwa watoto wenye mahitaji mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kurudisha kwa jamii.

Viti hivyo vimekabidhiwa kwa watoto hao katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kaulimbiu “Kwenda Extra Mile”, ambapo TANESCO imeamua kuifanya kaulimbiu hiyo ionekane kwa vitendo kupitia msaada unaolenga kuboresha maisha ya watoto wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf, amewataka wazazi na walezi kuhakikisha viti hivyo vinatunzwa ili viendelee kuwa msaada kwa watoto hao kwa muda mrefu.

DC Jamila amesema hatua hiyo haipaswi kuishia TANESCO pekee, bali iwe chachu kwa taasisi nyingine kuangalia namna zinavyoweza kutumia nafasi walizonazo kurudisha kwa jamii na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Kwa wazazi, msaada huo umeondoa sehemu ya mzigo waliokuwa wakibeba katika kuwapeleka watoto wao shule.

Lidia Sebastian, mmoja wa wazazi walionufaika, amesema kabla ya kupata kiti mwendo alikuwa akitumia hadi shilingi 60,000 kwa mwezi kumpeleka mtoto wake shule kwa bodaboda.

“Nilikuwa natumia hadi elfu sitini kwa mwezi kwa ajili ya usafiri wa mtoto kwenda shule. Hiki kiti kimetupunguzia gharama na kimetupa faraja,” amesema Lidia.

Kwa upande wake, TANESCO Mkoa wa Katavi imesema uamuzi wa kutoa msaada huo umetokana na dhamira ya kwenda “Extra Mile” kwa kuwafikia wananchi wenye mahitaji maalumu na kusaidia kuboresha mazingira yao ya maisha.

Kwa mujibu wa TANESCO, viti hivyo vitawasaidia watoto kupata usafiri salama zaidi, hasa wanapokwenda shule, huku vikiwa pia suluhisho kwa changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua.

Watoto waliopokea msaada huo wameishukuru TANESCO na kuiombea baraka, wakisema msaada huo umepunguza changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo katika usafiri.

Hatua hiyo ya TANESCO Katavi inaendelea kuonyesha nafasi ya taasisi katika jamii, ambapo huduma kwa wananchi inaweza kwenda sambamba na uwajibikaji wa kijamii na kurudisha kwa jamii, hasa kwa makundi yanayohitaji msaada zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.