Skip to main content

TANESCO KATAVI WAONGEZEWA VITENDEA KAZI

Na Daniel Gahu - Katavi.

TANESCO KATAVI WAONGEZEWA VITENDEA KAZI

Na Daniel Gahu - Katavi.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Katavi limekabidhiwa gari jipya aina ya crane lenye uzito wa tani kumi, ambapo limekabidhiwa kwa wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf Kimaro.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Ofisi ya TANESCO Mkoa wa Katavi, ambapo gari hilo litatumika katika shughuli za kunyanyua vifaa vizito kama mashine umba (transfoma), nguzo za zege, madramu ya nyaya na vitu vinginevyo jambo ambalo litakuwa suluhisho la changamoto ya muda mrefu ya hitaji la gari lenye uwezo huo Mkoani Katavi hususani ndani ya wilaya ya Mpanda.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Gari hilo, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amewataka viongozi wa TANESCO Mpanda na wafanyakazi wote kulitunza gari hilo pamoja na kuepuka tamaa ya kulitumia kinyume na malengo yake.

"Sisi binadamu tumekuwa haturidhiki na vitu tulivyonavyo, huwa tunakuwa na tamaa tamaa, hivyo dereva wa gari hili nikuombee kwa Mwenyezi Mungu akuondolee tamaa ya kubeba vitu visivyo hitajika katika gari hili kwani wananchi wetu wa hivi sasa wanauelewa, hivyo wanaweza wakahoji pindi wakiliona gari limebeba vitu vinginevyo tofauti na miundombinu ya shirika la umeme," amesema DC Jamila Yusuf.

Pia ameongeza, "hii itawezesha kutatua changamoto zinazokwamisha utoaji wa huduma bora ya umeme kwa wananchi wa Mpanda na kuendeleza tabasamu kwa wateja pamoja na wananchi wetu".

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ametoa wito kwa watumishi wa shirika hilo pamoja na wananchi wote kwa ujumla wa Manispaa ya Mpanda, kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa EBOLA ambao umezuka katika mipaka ya nchi jirani ya Congo DRC.

Pia amewataka watumishi wa shirika hilo kutenda kazi zao kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma ili kuepuka mambo yasiyofaa kama rushwa , ulevi, uzembe kazini, kwani kupitia mambo hayo huchangia kwa kiasi kikubwa malalamiko kwa wananchi wetu juu ya utendaji kazi kwa watumishi wa Umma.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Katavi, Mhandisi Florence Mwakasege, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwaletea vifaa na vitendea kazi, kwani inaongeza morali kwa watumishi katika kutoa huduma kwa wakati na kwa usalama zaidi.

Nao watumishi wa Shirika hilo la TANESCO Mkoa wa Katavi, wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan huku wakiahidi kulitunza na kulitumia gari hilo kulingana na malengo tarajiwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.