Skip to main content

TAMWA - ZNZ YAOMBA POLISI KUHARAKISHA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI RAIYAN

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kinaliomba Jeshi la Polisi kuharakisha uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa kidato cha kwanza Raiyan Hemed Amour (15), wa skuli ya Sekondari Kizimbani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambaye mwili wake ulidaiwa kukutwa katika kichaka huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa kimekatwa na kitu chenye ncha kali.

TAMWA - ZNZ YAOMBA POLISI KUHARAKISHA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI RAIYAN
Studio Narration JAMBO FM

TAMWA - ZNZ YAOMBA POLISI KUHARAKISHA UCHUNGUZI KIFO CHA MWA...

0:00 --:--

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kinaliomba Jeshi la Polisi kuharakisha uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa kidato cha kwanza Raiyan Hemed Amour (15), wa skuli ya Sekondari Kizimbani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambaye mwili wake ulidaiwa kukutwa katika kichaka huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa kimekatwa na kitu chenye ncha kali.

Kwa muijibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa 5, 2026, mwili wa Raiyan ulionekana katika kichaka akiwa amefariki dunia baada ya kuondoka nyumbani kwao, Kijiji cha Kwale Mpona siku ya Ijumaa Oktoba 2, 2026 majira ya saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya kwenda skuli.

"TAMWA ZNZ inaomba uchunguzi wa kina na haraka ufanyike ili kubaini mazingira ya kutoweka na hatimae kifo cha Raiyan, ili mtu au watu waliohusika na ukatili huo wanabainishwa na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi katika mifumo ya haki na ulinzi wa watoto," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, TAMWA-ZNZ imebainisha kuwa, hatua madhubuti dhidi ya wahusika zitatoa ujumbe wa wazi kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watoto havitavumiliwa katika jamii.

Juhudi kubwa zimekuwa zikifanywa na Serikali pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuimarisha haki za wanawake na watoto, hususan katika kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata fursa sawa za elimu, ulinzi na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii, baada ya kuachwa nyuma katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa muda mrefu.

Oktoba

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.