Ofisi ya Rais Tamisemi imeitunuku Halmashauri ya mji wa Mbulu Tuzo ya pongezi kwa kufikia kigezo kilichokubalika (KPI) cha Ufaulu wa mitihani wa Taifa wa kidato cha Nne 2025.
Halmashauri ya Mji wa Mbulu ni miongoni mwa Halmashauri kumi(10) ambazo zimefikia kiwango cha juu cha KPI kwa Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 ikiwa na asilimia 72 ambapo ndiyo Halmashauri ya Kwanza Kitaifa.
Tuzo hiyo ilitolewa Julai 18,2026 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Prof. Riziki Shemdoe.



Discussion
Reader comments
0 contributions