Skip to main content

TAMASHA LA UTAMADUNI KUANDIKA HISTORIA GEITA, RC SHIGELA AELEKEZA JAMBO

Na Ibrahim Rojala - Geita.

TAMASHA LA UTAMADUNI KUANDIKA HISTORIA GEITA, RC SHIGELA AELEKEZA JAMBO
Studio Narration JAMBO FM

TAMASHA LA UTAMADUNI KUANDIKA HISTORIA GEITA, RC SHIGELA AEL...

0:00 --:--

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ameitaka Manispaa ya Geita kujipanga vyema katika uratibu wa Tamasha la Utamaduni na Nyama Choma Manispaa ya Geita, ili kulifanya kuwa tukio kubwa la kihistoria kwa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Ameeleza hayo wakati akifungua tamasha hilo la siku mbili linalofanyika kati ya Mei 22-23,2026 katika viwanja vya maonesho vya Dkt .Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita ambapo amebainisha kwamba endapo likipangwa vyema litaweza kuvutia watalii wanaoingia nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela.

"Tukijipanga vizuri zaidi jambo hili linakwenda kuwa ni sehemu ya tukio kubwa la kihistoria katika mkoa wetu na nchi yetu, maana yake jambo hili litaweza kuunganisha hata wale watalii, watajua kuwa ukienda kwenye kutalii Tanzania,ukatembelea Serengeti ukitaka shughuli za sanaa utamaduni na nyama choma,nenda Geita Manispaa,” ameeleza.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Anglo Gold inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML), anayeshughulikia masuala ya Uendelevu na mambo ya Ubia,Bw Simon Shayo ameeleza umuhimu wa matamasha ya aina hiyo kwa kutolea mfano wa mabara ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiendesha shughuli zake  kuwa licha ya wafanyakazi kutoka katika jamii zenye  tamaduni mbalimbali bado wanafanikiwa kuishi pamoja kutokana na kutambua utajiri uliopo katika tamaduni.

“Kwenye jamii tunazofanya kazi,wengi wetu hapa Geita baadhi yetu ni wageni lakini kwakuwa tunafanya kazi hapa na kampuni inafanya kazi hapa tunajiona wenyeji wa Geita,hapa Geita Gold Mine Mheshimiwa mgeni rasmi tunajivunia kuakisi utofauti huo wa kimataifa,wafanyakazi wetu wanatoka maeneo mbalimbali,makabila na tamaduni mbalimbali,tunathamini utamaduni huu kwasababu unaimarisha ushirikiano,unatanua mtazamo,unachochea ubunifu na unasaidia kujifunza,” amesema Shayo.

Akizungumza katika Tamasha hilo kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Geita, Diwani wa Kata ya Nyankumbu ambaye pia ni Katibu wa Madiwani Manispaa ya Geita Paschal Kimisha Sukambi,amesema Manispaa ya Geita imeamua kutumia tamasha hilo kutunza  kumbukumbu ya maisha ya jamii ya Geita, ili kulinda utamaduni kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita,Yefred Myenzi.

“Hakuna utumwa mkubwa duniani kama watu kusahau walikotoka,leo  Mheshimiwa mkuu wa Mkoa tumeamua kuanza rasmi kutunza kumbukumbu ya maisha yetu na kama tutaendelea hivi,miaka hamsini ijayo wakati wengine wakisema utamaduni wetu umepotea,naamini Geita tunaweza kuweka mkakati mzuri wa watu kwenda kujifunza kujua baba zao na babu zao wametoka wapi,” amebainisha Diwani Sukambi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita,Yefred Myenzi amesema ni pamoja na kuwakumbusha wananchi na wadau mbalimbali umuhimu wa kuendeleza mila,desturi maadili na utamaduni mzuri uliokuwepo ndani ya jamii tangu enzi na enzi,kutengeneza fursa kwa wananchi, wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara kati kuonesha biashara zao na kujiingizia kipato.

Makamu wa Rais wa Anglo Gold i(GGML), Simon Shayo.

Myenzi amebainisha kwamba malengo mengine ni kutoa burudani kupitia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na kujenga na kuimarisha umoja,amani na mshikamano wa kijamii kati ya  wananchi na washiriki wa tamasha husika.

Amebainisha kwamba kupitia tamasha hilo, Halmashauri ya Manispaa ya Geita kupitia Idara ya utamaduni, sanaa na michezo imeratibu na kuwezesha utafiti juu ya chimbuko la makabila yanayoishi mkoani Geita kwa lengo la kuhifadhi taarifa zilizokusanywa na wenyeji na hasa wazee wa mila ambazo zina umuhimu wa kuendelea kutumika kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Diwani wa Kata ya Nyankumbu ambaye pia ni Katibu wa Madiwani Manispaa ya Geita Paschal Kimisha.

Tamasha hilo limeandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa ushirikiano na mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGML) likihusisha vipengele mbalimbali kama vile maandalizi ya vyakula vya asili,ngoma za asili,nyama choma na maonesho ya ujasiriamali kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali kujiingizia kipato.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.