Na Saulo Stephen - Singida.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imewapongeza wadau mbalimbali kwa ushirikiano waliouonyesha na kujitokeza katika hafla ya Maalumu ya Iftar iliyoandaliwa na taasisi hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Mjini Singida, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo, Petro Horombe amewapongeza kwa kujitokeza katika Iftar hiyo na kusisitiza ushirikiano wa wadau mbalimbali katika juhudi za kupinga Ruswa katika Mkoa wa Singida.

Amesema, ushirikiano wa wadau umekuwa chachu ya mafanikio katika mapambano dhidi ya rushwa na kuwataka kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo.
Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Singida, Sheikh Issa ibn Nassor , ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri wanayoifanya, huku akiishauri taasisi hiyo kupanua wigo wake kwa kufuatilia miradi inayotekelezwa na taasisi za dini, ili kuhakikisha uwajibikaji.


Discussion
Reader comments
0 contributions