Skip to main content

UBADHIRIFU MALI ZA UMMA: TAKUKURU YAOKOA MILIONI 624 KAGERA

Clavery Christian Bukoba - Kagera.

UBADHIRIFU MALI ZA UMMA: TAKUKURU YAOKOA MILIONI 624 KAGERA
Studio Narration JAMBO FM

UBADHIRIFU MALI ZA UMMA: TAKUKURU YAOKOA MILIONI 624 KAGERA

0:00 --:--

Clavery Christian Bukoba - Kagera.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 624 katika kipindi cha Julai 2025 hadi Mei 2026 kupitia juhudi zake za kupambana na vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Leonard Swai amesema mafanikio hayo yametokana na usimamizi madhubuti wa sheria pamoja na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi katika kutoa taarifa za vitendo vya rushwa.

Amesema kuwa katika kipindi hicho, kesi 61 zilifikishwa mahakamani ambapo kesi 52 ziliamuliwa na TAKUKURU kushinda kesi 50, hali ambayo imeonesha uimara wa ushahidi pamoja na weledi wa maafisa wake katika uendeshaji wa mashauri ya rushwa.

Swai, amesema TAKUKURU imeendelea kufuatilia matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 2.2 katika utekelezaji wa miradi 29 ya maendeleo huku akitoa ushauri kwa wataalam na wasimamizi wa miradi kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha iliyotengwa.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kuendelea kujiepusha na vitendo vya rushwa akisisitiza kuwa rushwa hailipi bali husababisha hasara kubwa kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Swai, taasisi hiyo itaendelea kusimamia misingi ya uwajibikaji, uadilifu na uzalendo ili kuhakikisha rasilimali za umma zinalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.