Skip to main content

TAKUKURU YAIBUA UBADHILIFU MIRADI 102 SIMIYU

Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.

TAKUKURU YAIBUA UBADHILIFU MIRADI 102 SIMIYU

Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.

Taasisis ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Simiyu imefanya ufuatiliaji wa wa miradi 102 inayotekelezwa mkoani humo na yenye thamani ya shilingi Bilioni 63 na kubaini kuwepo kwa  mianya katika uwasilishwaji wa bei kwa wazabuni, ambazo zimebainika kuwa kubwa kuliko bei halisi ya soko pamoja na ucheleweshwaji wa muda wa utekelezaji wa miradi bila kuwepo kwa sababu za msingi.

Akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika warsha ya wadau na wasimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoa wa Simiyu, Naibu Mkuu wa TAUKURU mkoani humo, Aaron Misanga amesema, kati ya miradi iliyochunguzwa miradi 14 kati yake imebainika kuwa na viashiria vya rushwa moja kwa moja.

“Kati ya miradi 102 ambayo tumeichunguza kwa kina miradi 14 tumebaini viashiria vya wazi vya rushwa na miradi  40 kati ya 102 ambayo nayo tumeiona ina mapungufu tumetulazimika kufanya majadiliano na baada ya hapo tumeelekeza miradi hiyo ifanyiwe marekebisho tofauti na vile ambavyo tumeona,na hii itasaidia kurudisha thamani ya fedha ambayo imewekwa kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi hiyo kwa maendeleo ya wananchi wetu,” amesema Aaron Misanga.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Simiyu, Manyama Tungaraza ametoa wito kwa wadau hao kuhakikisha pesa ambayo inatolewa kwa ajili ya utelekezaji wa miradi ya wananchi ifanyiwe usimamizi mzuri na viongozi hao ili isichangie kuzorota kwa maendeleo.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa rasilimali zinazotolewa na serikali pamoja na wadau wa maendeleo zinatumika kwa ufanisi na kuona kila mdau anashiriki katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo niwaombe viongozi wetu tusimamie hizi rasilimali kwa uchungu kwa ajili ya taifa letu,” amesema Manyama.

Ujumbe huo, umepokelewa vyema na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha ambaye ametoa maelekezo kwa watendaji wa taasisi zote za serikali na wadau mkoani humo kuhakikisha kunakuwepo na uwajibikaji katika kushiriki kufuatilia miradi ya maendeleo bila msukumo.

“Ni muhimu kujua kuwa maendeleo ya mkoa wetu yanategemea uwajibikaji na ushiriki katika usimamizi wa miradi yetu ili malengo yaliyowekwa yanafikiwa naimani kubwa kuwa tukifanya kazi kwa kushirikiana uaminifu bila kusukumwa na mtu yoyote basi lazima tutafanikiwa kudhibiti huu ubadhilifu ambao unataka kuturudisha nyuma,” amesema RC Macha.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.