Skip to main content

TAKUKURU YABAINI MAPUNGUFU YA MIRADI, YAOKOA MAMILIONI GEITA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

TAKUKURU YABAINI MAPUNGUFU YA MIRADI, YAOKOA MAMILIONI GEITA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Mkoa wa Geita imebaini mapungufu katika miradi mitatu kati ya 17 iliyofanyiwa uchunguzi ndani ya kipindi cha kati ya Oktoba-Desemba 2025.

Kwa ujumla ndani ya kipindi hicho, TAKUKURU mkoa wa Geita  imefanikiwa kurejesha kiasi cha sh 94,211,596 katika udhibiti wa miradi ya Maendeleo na uchunguzi wa mashtaka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya  vya habari Machi 27,2026 na Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita,Alex Mpemba,Taasisi hiyo katika kipindi hicho ilifanikisha malipo ya kiasi cha sh 25,200,000 yasilipwe kutokana Mkandarasi Kuweka kifusi cha udongo wa mfinyanzi katika barabara iliyopo halmshauri ya wilaya ya Geita eneo la Nzera kuelekea makutano ya barabara ya Nzera na Nkome hatua iliyomlazimu mkandarasi kurudia kazi kwa kuweka kifusi cha Moram kama ilivyoelekezwa.

Katika kipindi hicho pia,kiasi cha shilingi 32,037,000 kilirejeshwa kwenye mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) baada ya mshtakiwa kumuongezea mnufaika asiyestahili aliyepata matibabu ya kiasi hicho isivyo halali.

Taasisi hiyo pia ilisaidia kurejesha kiasi cha Shilingi 300,000 ambazo zilikuwa za manunuzi ya kompyuta katika kituo cha afya Nyabirezi-Chato baada ya mhusika kutowasilisha kompyuta hiyo katika kituo hicho.

Kiasi cha shilingi 20,020,000 kilirejeshwa katika akaunti ya AMCOS ya Idoselomwalo iliyopo CRDB Mbogwe baada ya AMCOS hiyo kuchukua mkopo wa Shilingi milioni 245 katika benki ya CRDB na kutourejesha,wakati fedha za mapato kiasi cha shilingi 8,142,900 kilirejeshwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Geita,shilingi 154,100 zikirejeshwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nyangh'wale, ambazo ni fedha za mapato yaliyokusanywa kwa mashine ya POS na kutowasilishwa benki na wakusanya mapato.

Tasisi hiyo pia katika kipindi hicho ilifanikiwa kurejeshwa kwa kiasi cha shilingi 3,227,087.83 na shilingi 2,436,852 zilizowekwa katika akaunti ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato, zikiwa ni fedha za mapato ya Service Levy ambazo hazikulipwa na wakandarasi waliopata kazi TANROADS na RUWASA katika wilaya ya Chato.

Katika hatua nyingine TAKUKURU mkoa wa Geita ndani ya kipindi hicho cha Oktoba-Disemba 2025, ilifuatilia matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kumi na saba (17) yenye thamani ya Shilingi 58,015,449,352.26, miradi 14 kati ya 17 ilibainika kuwa na mapungufu madogo,miradi mitatu ikibainika kuwa na mapungufu makubwa hali iliyolazimu kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kunusuru miradi hiyo ikiwemo kuwelekeza wakandarasi kurudia ujenzi katika sehemu zenye mapungufu kwa gharama zao.

Sambamba na hayo jumla ya malalmiko 49 yalipokelewa na Taasisi hiyo, malalamiko 38 ambayo ni sawa na asilimia 78 yalihusu makosa ya rushwa, malalamiko 11,ambayo ni sawa na asilimia 22 hayakuhusu makosa ya rushwa,kesi 5 ziliamuliwa ambapo Jamhuri ilishinda kesi 4 na kesi nane (8) bado zinaendelea katika mahakama mbalimbali za mkoa wa Geita.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.