Skip to main content

TAKUKURU TABORA WAKABIDHI VIFAA TIBA UHUDUMIAJI WATOTO NJITI

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Neema Mwakalyelye, amewaongoza watumishi wa taasisi hiyo Mkoa wa Tabora kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

TAKUKURU TABORA WAKABIDHI VIFAA TIBA UHUDUMIAJI WATOTO NJITI

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Neema Mwakalyelye, amewaongoza watumishi wa taasisi hiyo Mkoa wa Tabora kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. 

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora–Kitete, mbele ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Upendo Wella. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Upendo Wella amewapongeza watumishi wa TAKUKURU kwa moyo wa kujitolea na kuchanga fedha zao kununua vifaa hivyo, akisema hatua hiyo ni mfano mzuri kwa watumishi wa umma na wadau wengine kushiriki katika kusaidia jamii na kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. 

“Pamoja na kutekeleza majukumu yetu ya kawaida, tunao wajibu wa kusaidia jamii inayotuzunguka. Serikali imeendelea kufanya kazi kubwa, lakini nchi yetu ni pana na mahitaji ni mengi; hivyo, nawasihi watumishi na wadau wa kada mbalimbali kuunga mkono juhudi hizi,” amesema DC Wella.

Kwa upande wake, Bi. Mwakalyelye amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni Infant Radiant Warmer na Phototherapy Unit, huku Hospitali ya Kitete ikiwa miongoni mwa hospitali za rufaa zilizofikiwa na mpango huo nchini. 

Ameeleza kuwa hadi kufanyika kwa makabidhiano hayo, TAKUKURU ilikuwa imekabidhi jumla ya mashine 25, huku Tabora ikiwa mkoa wa 23 kufikiwa na msaada huo.

Bi. Mwakalyelye amefafanua kwa kusema "fedha zilizotumika kununua vifaa hivyo hazikutokana na bajeti ya utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU, bali ni michango ya hiari ya watumishi wake."

Amesema hatua hiyo ni ishara ya upendo kwa jamii na inaunga mkono jitihada za serikali katika kuimarisha huduma za afya, hususan afya ya mama na mtoto. 

Akitoa salamu kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bi. Makuri Kambarage ameishukuru TAKUKURU kwa mchango huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kusaidia sekta ya afya.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora–Kitete, Dkt. Joachim Eyembe, amesema msaada huo ni wa kihistoria na utasaidia kuimarisha huduma pamoja na kuokoa maisha ya watoto Njiti.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.