Skip to main content

TAKUKURU SHINYANGA YAREJESHA ZAIDI YA TSHs MIL. 21 ZA MIRADI

Na Eunice Kanumba –Shinyanga

TAKUKURU SHINYANGA YAREJESHA ZAIDI YA TSHs MIL. 21 ZA MIRADI

Na Eunice Kanumba –Shinyanga

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kusaidia kurejeshwa kwa zaidi ya Shilingi milioni 21 katika kipindi cha Januari hadi Machi 2026 kupitia ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma, uchunguzi wa tuhuma za rushwa pamoja na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akizungumza leo tarehe 29 may 2026 kuhusu mafanikio hayo, ya TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga mkuu wa taasisi hiyo Donasian Kessy amesema   kuwa jumla ya Shilingi 21,897,954/= zimerejeshwa baada ya kubainika kuwepo kwa dosari mbalimbali katika matumizi na usimamizi wa fedha za umma.

Miongoni mwa fedha zilizookolewa ni Shilingi 5,540,254/= zilizopatikana kupitia ufuatiliaji wa mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Awali na Msingi Tinde “B” uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Katika ufuatiliaji huo, ilibainika kuwa kiasi cha Shilingi 5,316,304/= kilipaswa kulipwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kama kodi ya zuio (withholding tax), huku Shilingi 223,950/= zikiwa ni ushuru wa huduma ambao haukulipwa kwa wakati stahiki.

TAKUKURU imeeleza kuwa hatua hizo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha uwajibikaji, uwazi na matumizi sahihi ya fedha za umma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha, taasisi hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali ili kuhamasisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma na kuanisha kuwa taasisi hiyo  imefanikiwa kutoa mafunzo kwa njia ya semina wa viongozi vyama vya msingi  vya kilimo na masoko (AMCOS) wa wilaya ya Kishapu mafunzo ambayo yamewezesha AMCOS zinazodaiwa na makampuni ya ununuzi wa pamba kurejesha fedha kiasi cha shilingi 9,322,000 walizokuwa wakidaiwa  na makampuni hayo.

Kessy ametoa  wito kwa taasisi zote za umma kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya maadili lakini pia wananchi wa mkoa amewaomba kushirikiana kikimilifu na taaisis hiyo katika juhudi za kupambana na rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii kwa ujezi wa taifa la Tanzania.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.