Skip to main content

TAIWAN KUNUNUA SILAHA ZA KUJILINDA DHIDI YA CHINA

Serikali ya Taiwan imethibitisha kuendelea na mazungumzo ya kimkakati na Marekani juu ya ununuzi wa silaha za kijeshi,

TAIWAN KUNUNUA SILAHA ZA KUJILINDA DHIDI YA CHINA
Studio Narration JAMBO FM

TAIWAN KUNUNUA SILAHA ZA KUJILINDA DHIDI YA CHINA

0:00 --:--

Serikali ya Taiwan imethibitisha kuendelea na mazungumzo ya kimkakati na Marekani juu ya ununuzi wa silaha za kijeshi,

Waziri wa Ulinzi wa Taiwan, Wellington Koo, amebainisha hay oleo jumanne akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la bunge mjini Taipei. Akibainisha kuwa Taiwan imepokea maelezo ya wazi kutoka kwa serikali ya Marekani baada ya mkutano huo wa kilele, ikisisitizwa kuwa msimamo wa Marekani wa kuisaidia Taiwan haujayumba.

"Kuhusu mauzo ya zana za kijeshi yanayoendelea, bado tuko kwenye mazungumzo ya mara kwa mara na upande wa Marekani. Kila mradi unahitaji ushirikiano wa karibu. Kwa uelewa wangu, hadi sasa hatujapokea taarifa yoyote ya mabadiliko," alisema Koo.

Marekani inasalia kuwa msaidizi mkuu wa kimataifa na msambazaji mkubwa wa silaha kwa Taiwan, licha ya kutokuwa na uhusiano rasmi wa kidiplomasia.

China, inayokichukulia kisiwa cha Taiwan kuwa sehemu ya eneo lake, imekuwa ikitaka Marekani isitishe mara moja mauzo ya silaha kwa serikali ya Taipei. Baada ya ziara yake mjini Beijing mwezi Mei.

Hata hivyo Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa anazuia kwa muda kifurushi kipya cha silaha za kijeshi chenye thamani ya takriban dola bilioni 14.

kufuatia mkutano wake na Rais wa China Xi Jinping mjini Washington, Trump alidokeza kuwa kiongozi huyo wa China anaelewa msimamo wake kuhusu Taiwan.

Kwa sasa, Taiwan inakabiliwa na kucheleweshwa shehena za silaha zilizokuwa imeahidiwa na kuagiza awali. Huku miongoni mwa ucheleweshaji mkubwa ni agizo la mwaka 2019 la ndege za kivita 66 aina ya F-16V kutoka kampuni ya Lockheed Martin.

Kadharika Ndege hizo zimeratibiwa kuimarishwa kwa mifumo ya kisasa ya kielektroniki na rada ili kuongeza uwezo wa Taiwan kukabiliana na jeshi la anga la China, ikiwemo ndege zake za kisasa za J-20.

Wakatin hayo yanajiri Vyombo vya habari nchini Taiwan vimeripoti kuwa ndege mbili za kwanza aina ya F-16V ziko nchini Hawaii zikisubiri kusafirishwa.

Hata hivyo Waziri Koo alikana kuzungumzia kwa undani ratiba ya uwasilishaji huo, akisema mchakato wa uzalishaji umefikia hatua inayowezesha uwasilishaji, na kwamba kuna hatua za fidia zinazochukuliwa kutokana na kuchelewa huko.

"Tutaendelea kuratibu mambo na upande wa Marekani kuhusu uwasilishaji huo," aliongeza Koo. Kampuni ya Lockheed Martin haijatoa maelezo yoyote hadi sasa.

Chini ya Sheria ya Uhusiano na Taiwan ya mwaka 1979 (Taiwan Relations Act), Marekani inawajibika kisheria kuipatia Taiwan njia na zana za kujilinda dhidi ya tishio lolote.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.