Skip to main content

TAHARUKI TETEMEKO LA ARDHI BAADHI YA MAENEO TANZANIA, NCHI JIRANI

Tetemeko la ardhi limetikisa mkoa wa Geita leo mchana na kuhisiwa katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kahama na hata nchi jirani za Rwanda, Kenya na Uganda.

TAHARUKI TETEMEKO LA ARDHI BAADHI YA MAENEO TANZANIA, NCHI JIRANI

Tetemeko la ardhi limetikisa mkoa wa Geita leo mchana na kuhisiwa katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kahama na hata nchi jirani za Rwanda, Kenya na Uganda.

Kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Kijiolojia la Marekani (USGS) na Kituo cha Ulaya cha Kutetemeka (EMSC), tetemeko hilo limetokea hii leo majira ya Saa: 12:22 mchana.

Eneo: Kilomita 21 Mashariki mwa Ushirombo, Bukombe - Geita

Ukubwa: 5.1 - 5.2 kwenye kipimo cha Richter (Awali iliripotiwa 5.6)

Kina: Kilomita 10 tu chini ya ardhi na ndio maana limehisiwa mbali, kwa sababu ni tetemeko la kina kifupi.

Mitetemo yake pia imesikika mpaka Kigali, Rwanda - kilomita 292 kutoka chanzo chake na hadi Nairobi, nchini Kenya.

NINI KIMETOKEA.

Wafanyakazi waliokuwa kwenye majengo ya ghorofa jijini Mwanza walilazimika kukimbilia nje ya ofisi zao baada ya kuhisi majengo yakitikisika kwa sekunde kadhaa.

Taharuki ilitanda kwa muda mfupi kabla ya watu kurejea kwenye shughuli zao.

Hadi sasa, hakuna taarifa za vifo, majeruhi wala uharibifu mkubwa ulioripotiwa na Mamlaka husika bado zinafuatilia.

KWANINI TETEMEKO LIMEPITA TANZANIA.

Tanzania ipo kwenye Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East African Rift Valley) , eneo linaloendelea kupasuka taratibu.

Ndio maana mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Mara hupata matetemeko mara kwa mara.

Mwezi uliopita, Oktoba 9, tetemeko la 5.0 lilitokea Kagera, na mwaka 2016 tetemeko la 5.7 liliikumba Kagera na kuleta madhara.

TAHADHARI.

Wakati wa tetemeko Wataalamu wanashauri mambo yafuatayo-.

i. Kaa mbali na majengo marefu wakati wa tetemeko

i. Usitumie lifti

iii. Kama uko ndani, jifunike chini ya meza imara

iv. Kaa tayari kwa mitetemo ya baadaye (aftershocks)

Jambo FM tutaendelea kukupa taarifa mpya kadri zinavyokuja.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.