Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuonekana kwa jeneza dogo lililotelekezwa katika uwanja wa Soko la Mnada Kabila, lililopo Kata ya Kabila, Wilaya ya Magu.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo, imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Juni 29, 2026 majira ya saa 11.00 alfajiri, baada ya wananchi kuripoti uwepo wa jeneza hilo.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa jeneza hilo lilikuwa na rangi ya zambarau na msalaba wenye rangi nyeupe. Ndani ya jeneza hilo vilikutwa vipande vya nyama, kichwa na miguu ya kondoo, pamoja na dawa za kienyeji," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoani humo limewakata wananchi wa Kata ya Kabila na maeneo jirani, kuwa watulivu na kutokuwa na imani potofu za kishirikina, likiarifu kuwa vitendo vyovyote vya kuwashambulia watu kwa tuhuma za ushirikina, ni kinyume na sheria.


Discussion
Reader comments
0 contributions