Wirlzara ya Afya Nchini Uganda, imesema itawaweka karantini kwa siku 21 raia wake wanaorejea nchini humo kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Uamuzi huo, umetangazwa hii leo Oktoba 25, 2026 na Waziri wa Afya wa Uganda, Chris Baryomunsi ambaye amesema unatokana na uimarishaji wa tahadhari za Ebola.

Hayo yanajiri wakati Uganda ikichunguza kisa cha Ebola cha Nigeria, kinachomhusisha mwanamke mmoja aliyesafiri kutoka Uganda kuelekea Taifa hilo.
Hqta hivyo, Baryomunsi amesema tayari watu wote 60 waliogusana na mgonjwa wa Ebola wa Kenya, wamekamilisha kipindi chao cha uangalizi wa siku 21 na wameruhusiwa.
Discussion
Reader comments
0 contributions