Skip to main content

TABORA YAWEKA MIKAKATI KUZIKABILI ATHARI ZA EL-NINO

Mkoa wa Tabora umeanza kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño, kwa kuimarisha ushirikiano wa taasisi za Serikali na jamii katika hatua za tahadhari na mwitikio wa majanga.

TABORA YAWEKA MIKAKATI KUZIKABILI ATHARI ZA EL-NINO
Studio Narration JAMBO FM

TABORA YAWEKA MIKAKATI KUZIKABILI ATHARI ZA EL-NINO

0:00 --:--

Mkoa wa Tabora umeanza kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño, kwa kuimarisha ushirikiano wa taasisi za Serikali na jamii katika hatua za tahadhari na mwitikio wa majanga.

Hatua hiyo imejadiliwa katika kikao maalum cha Kamati ya Wataalamu ya Mkoa ya Usimamizi wa Maafa kilichofanyika katika Ukumbi wa TACTIC, Tabora.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, na kushirikisha Makatibu Tawala wa Wilaya zote za mkoa huo, watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Mboya amezitaka Halmashauri zote za Wilaya kuunda kamati ndogo za kisekta zitakazokuwa na jukumu la kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

Amesema maandalizi ya mapema ni muhimu katika kupunguza madhara ya majanga, huku akisisitiza umuhimu wa kila sekta kuwa na mpango madhubuti wa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika maeneo yao.

Aidha, Dkt. Mboya ameielekeza Kamati ya Wataalamu ya Mkoa ya Usimamizi wa Maafa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na njia nyingine za mawasiliano.

Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kupata taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa mvua, kutambua athari zinazoweza kujitokeza na kuchukua hatua stahiki za tahadhari, sambamba na kusaidia kudhibiti kuenea kwa taarifa zisizo sahihi.

Kwa upande wao, Makatibu Tawala wa Wilaya wamewasilisha taarifa kuhusu hali ya maandalizi katika maeneo yao, ikiwemo hatua zinazochukuliwa kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya taasisi za Serikali, viongozi wa maeneo na wananchi.

Mikutano na maandalizi hayo yanaendelea kuwa sehemu ya hatua za Mkoa wa Tabora kuhakikisha kuwa mifumo ya tahadhari, kinga na mwitikio wa majanga inawekwa katika hali ya utayari kabla na wakati wa mvua.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.